Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na. bilson vedastus - Dodoma
Naibu Waziri Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya Nishati
Mhe. Charles Kitwanga amefanya ziara ya kutembelea Bwawa la kuzalisha
Umeme la Mtera mwishoni mwa wiki kwa lengo la kuangalia mwenendo wa maji
katika bwawa hilo.
Wakati akizungumza na watendaji wa Bwawa hilo,
Kitwanga amewataka watendaji hao kuhakikisha kuwa Bwawa la Mtera
linaendelea kuwa na kiasi cha maji ya kutosha wakati wote ili kuweza
kuzalisha umeme wa kutosha.
Aidha, ameongeza kuwa, uzalishaji umeme
kwa njia ya maji ni muhimu kutokana na gharama zake kuwa nafuu
ikilinganishwa na gharama za kuzalisha umeme unatokana na gesi au vyanzo
vingine. Hivyo, amewataka wananchi wanaofanya shughuli zao jirani na
vyanzo vya maji kuhakikisha wanavilinda kwa ajili ya maendeleo na
manufaa ya taifa.
Katika hatua nyingine amewataka watendaji hao
kufikiria vyanzo vingine vya kuzalisha umeme mbali na gesi badala ya
kusubiri rasilimali ya gesi pekee kuweza kuzalisha umeme.
Aidha
ameeleza kuwa, wananchi wana matarajio makubwa na nishati ya umeme
hivyo, amewataka watumishi wa Wizara ya Nishati na Madini kufanya kazi
kwa bidii kwa ajili ya kuwatumikia watanzania huku wakitanguliza
uzalendo.
Home »
» WAZIRI WA NISHATI NA MADINI ATEMBELEA BWAWA LA KUZALISHA UMEME LA MTERA
0 comments:
Post a Comment