Home » » MKURUGENZI MJI MAFINGA AHIMIZA WATUMISHI KUFANYA KAZI KWA KUELIMISHANA NA USHIRIKIANO

MKURUGENZI MJI MAFINGA AHIMIZA WATUMISHI KUFANYA KAZI KWA KUELIMISHANA NA USHIRIKIANO

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mji Mafinga Bi Fidelica Myovella alipokutana na watumishi wa Halmashauri ya Mji Mafinga kuwasikiliza na kutatua changamoto zao katika kikao kilichofanyika katika Shule ya Sekondari JJ Mungai Mafinga.

“ Kila mmoja akitimiza wajibu wake kwa kazi aliyopewa na Serikali hakutakuwa na kukomoa kwenye utendaji wetu wa kazi, tutafanya kazi kwa kutii Mamlaka iliyopo na tutakusanya mapato kwani ni jukumu letu sote, kwa kukusanya mapato vizuri tutatekeleza miradi ya Maendeleo na wananchi tunaowatumikia watapata huduma bora na kwa uharaka”

Bi Fidelica Mnyovella amesema  wananchi wanapohudumiwa kwa lugha nzuri wanaisemea vyema Serikali inayowaongoza ameongeza kuwa kwa mwaka wa fedha 2023/2024 Halmashauri ya Mji Mafinga imevuka lengo la ukusanyaji mapato kwa asilimia 113 hadi kufikia june, kwa kukusanya Bilioni 6.2

“tusiwaongezee maumivu wananchi kwa kuwapokea kwa lugha mbaya kwani wanatutegemea katika kupata haki, tutumie lugha rafiki katika kutoa huduma kwa kufanya hivyo Serikali itasemewa vizuri na wananchi hao.”

Kikao hicho kimehudhuriwa na watumishi 133 wakiwemo Wakuu wa Idara na Vitengo, Walimu wakuu, Wakuu wa Shule, Maafisa Ugani wa sekta zote, Maafisa Elimu Kata, Watendaji wa Kata zote 9 na watumishi wa Ofisi Kuu ya Mji Mafinga.

Mada mbalimbali zimewasilishwa na wataalamu ikiwamo , Taarifa ya Utumishi, Maadilli na Itifaki, Mipango Miji na Ardhi pamoja na PEPMIS

Imeandaliwa na Kitengo Cha Mawasiliano Serikalini- Mafinga TC

Sima Bingileki
Mkuu wa Kitengo Cha Mawasiluano Serikalini- Mafinga TC

 

0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Iringa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa