Home » » KUTOKA MUFINDI: 'UKIKOSA MKOPO AWAMU HII SUBIRI' - DC MUFINDI

KUTOKA MUFINDI: 'UKIKOSA MKOPO AWAMU HII SUBIRI' - DC MUFINDI

“Nawaomba sana Sikilizeni vigezo vilivyowekwa, umekosa awamu hii awamu ijayo hakikisha unapata kwa kufuata vigezo vilivyowekwa,tusiwe wabishi lazima tufuate vigezo.
Fedha zinatolewa kila baada ya miezi mitatu kama umekosa awamu hii hakikisha unafuata vigezo na kuandika andiko vizuri ili upate mkopo kwa awamu inayofuata” DC- Mufindi Mheshimiwa Dkt Linda Salekwa.

Mhe. Linda amesema Serikali ipo kusimamia kila mwenye vigezo vya kupata mkopo anapata  na kuhakikisha haki inatendeka kwa kila muombaji, wa Mikopo hii ya asilimia 10.

Amesema Lengo la Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ni Kuhakikisha mikopo inawanufaisha wananchi waliolengwa ili kuwainua kiuchumi, 

“Naomba niwatoe hofu mikopo hii kwa awamu tunayotoa imepitiwa na kamati mbalimbali ikiwemo kamati ya Ulinzi ya Wilaya , ile dhana ya kupeana mikopo haipo”

 Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mheshimiwa Dkt. Linda Salekwa amechukua uamuzi wa kuwaita na kuwapa elimu wananchi wa Wilaya ya Mufindi waliokosa mkopo wa asilimia 10% ili kuwafafanulia vigezo vya mikopo ili awamu inayofuata waweze kupata mikopo hiyo isiyo na riba.

Sima Bingileki
Afisa Habari Mkuu- Mafinga TC


0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Iringa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa