Home » » KUTOKA JIMBO LA MAFINGA: MBUNGE WA JIMBO LA MAFINGA AKABIDHI MITUNGI 60 YA GESI KWA WATENDAJI WA KATA

KUTOKA JIMBO LA MAFINGA: MBUNGE WA JIMBO LA MAFINGA AKABIDHI MITUNGI 60 YA GESI KWA WATENDAJI WA KATA

“Lengo la kugawa nishati hii safi ya kupikia ni kuunga mkono juhudi za Kinara wa Nishati Safi ya Kupikia Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi. Nategemea Watendaji wa Kata Mitaa na Vijiji ndo wenye watu hadi ngazi ya chini kupitia njia hii watakuwa mabalozi wazuri wa matumizi ya nishati safi ya kupigia.”

Kauli hiyo imetolewa na Mbunge Wa Jimbo la Mafinga Mjini na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje Mheshimiwa Cosato Chumi alipokuwa akikabidhi mitungi 60 ya gesi kwa Watendaji wa Kata, Mitaa na Vijiji wa Jimbo la Mafinga Mjini lengo likiwa ni kusambaza matumizi Ya Nishati Safi ya kupikia na kuunga mkono juhudi za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kinara wa Nishati Safi ya kupikia.

Amewataka watendaji hao wakawe mabalozi wazuri wa Nishati Safi ya Kupikia ili kuwaokoa wakina mama wanaotumia masaa 4 vijijini kutafuta nishati za kupikia kama kuni kulingana na tafiti, huku tukilenga kuokoa mabadiliko ya tabia nchi yanayotokana na ukataji wa miti kusiko na mpangillio.

Aidha amewaasa watumishi hasa wa ajira mpya kufanya kazi kwa uvumilivu, kuchukuliana na kufuata kanuni kwani utumishi wa Umma hautaki haraka”

Niwaombe sana watumushi hakikisheni mnawatumikia
Wananchi na kuwa sehemu yao, kuweni wepesi kujifunza mjue tamaduni za watu mnaowaongoza na kuwa wanyenyemevu.

Hafla hiyo fupi imehudhuriwa na Mwenyekiti wa Mji Mafinga Mheshimiwa Regnant Kivinge, Kaimu Mkurugenzi Mji Mafinga Dorothy Kobelo, Wakuu wa Idara na wataalamu
Kutoka. Kampuni ni Lake Gas

Sima Bingileki
Mkuu wa Kitengo Mji Mafinga


0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Iringa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa