Home » » KUTOKA MUFINDI: MKUU WA WILAYA YA MUFINDI DKT LINDA SELEKWA AZINDUA ZOEZI LA UGAWAJI WA MIKOPO YA ASILIMIA KUMI HALMASHAURI YA MJI MAFINGA

KUTOKA MUFINDI: MKUU WA WILAYA YA MUFINDI DKT LINDA SELEKWA AZINDUA ZOEZI LA UGAWAJI WA MIKOPO YA ASILIMIA KUMI HALMASHAURI YA MJI MAFINGA


Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mheshimiwa Dkt Linda Selekwa  amezindua zoezi la ugawaji wa mikopo ya asilimia kumi kwa vikundi 62 vya wanawake ,vijana na watu wenye ulemavu katika Halmashauri ya Mji Mafinga ambapo jumla ya shilingi milioni 895,367,600 zimetolewa kwa vikundi hivyo.
Mheshimiwa  Dkt Linda Selekwa amewataka wanufaika wa mikopo hiyo kuhakikisha wanatumia fedha hizo katika kukuza na kuendeleza biashara na miradi ambayo wamekuwa wakiifanya na kuachana kujaribu kufanya kitu kipya ambacho kitawapotezea fedha hizo kwa sababu fedha hizi ni za Serikali na zinatokana na mapato ambayo tunalipa kwenye Halmashauri hivyo tunawajibu wa kusimamia kwa uwangalifu mkubwa ili ziweze kutukwamua kiuchumi na kuhimarisha hali ya kipato chetu ili tuweze kuondokana na umaskini.

Aidha amewakumbusha wanufaika wa mikopo ya vikundi vya wanawake, vijana, na watu wenye ulemavu umuhimu wa kulipa mapato ya Halmashauri ili kuongeza wigo wa vikundi vingine kupata mikopo na pia kuhakikisha vikundi vinarejesha mikopo hiyo kwa muda ambao umepangwa ili kuondokona na usumbufu ambao utaweza kujitokeza wakati wa marejesho hayo.

Kwa upande mwengine Mheshimiwa Dkt Linda Selekwa amevisisitiza vikundi ambavyo vimepata mikopo hiyo vinakuwa imara na kusimamia na kutekeleza  mambo ambayo wamepanga kuyafanya na pia kuepuka migogoro ambayo imekuwa inajitokeza katika vikundi hivyo na endapo ikitokea hivyo basi ofisi za Serikali ziko  wazi kwaajili ya kushuglikia migogoro hiyo ya vikundi na pia amehaidi vikundi ambavyo vitafanya vizuri vitapitiwa na Mwenge wa Uhuru na kuangalia shughuli zao.




0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Iringa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa