TONE

TONE

DC KASESELA AWATAKA WANANCHI KUACHANA NA IMANI ZA KISHIRIKINA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Pokea code:
 Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake hii leo

Na Fredy Mgunda,Iringa

Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela amewataka wananchi wa wilaya ya iringa kuacha tabia ya kuamini na kujihusisha na maswala ya imani za kishikina pamoja na kujichukulia hatua mikononi.

Ameyasema hayo baada ya kuwepo kwa taarifa za mtu mmoja mkazi wa kijiji cha mikong’wi kata ya kihologota wilaya ya iringa ameuawa na watu wasiojulikana kwa kukatwa kichwa na kutelekeza kiliwili chake.

“Kwanini watu wajichukulie hatua mkononi wakati serikali,jeshi la polisi,mahakama,makanisa na misikiti huku ndio unaweza kutatuliwa shida zako zote  na haya mambo ya kishikina serikali haiamini da nasikitika sana kwa tukio la leo ni baya sana”alisema Kasesela

Kasesela alisema kama wilaya wamepokea taarifa hiyo kwa masikitiko na kuwataka wananchi wote kutojichukulia sheria mikononi kwa kuwa serikali haiamini uchawi na kwamba ameliagiza jeshi la polisi kufanya uchunguzi ili kubaini aliyehusika na tukio hilo.

“Wilaya ya Iringa ilikuwa imetulia sasa yameanza mambo ya kuuwana kwa keli lazima jeshi la polisi lifanye uchunguzi kwa kina kubaini nini kinachoendelea katika kijiji cha mikong’wi na lazima tukomeshe na kuwa elimu wananchi kutojihusisha na maswala ya kishirikina kwa kuwa serikali haiamini sala hilo”alisema Kasesela 

Kasesela ameeleza kuwa tukio hilo limetokea asubuhi ya leo na kumtaja aliyefariki dunia kuwa ni hasani nyalusi mkazi wa kijiji cha mikong’wi tarafa ya Isman mkoani Iringa.

Aidha Kasesela amewaomba viongozi wa dili mbalimbali kutoa elimu ya mungu na kukemea maswala ya kishikina kwa kuwa yanapunguza nguvu kazi za wananchi.


Kwa upande wake afisa mtendaji wa kijiji cha Mikong’wi Majorino Muyinga Anaeleza kuwa Mnamo tarehe 06/04/2017 huko kitongoji cha Utitiri kijiji cha Mikong’wi kata ya Kihorogota tarafa ya Isimani wilaya ya Iringa vijijini Mkoani Iringa alisema kuwa Hassan Nyalusi alikutwa akiwa ameuawa nje ya nyumba yake na mtu/watu wasiofahamika na mwili ukiwa hauna kichwa na uchunguzi wa daktari umefanyika na kukabidhiwa kwa ndugu wa marehehemu kwa taratibu za mazishi laiki mtu mmoja Jackson Nyalusi anashikiliwa na polisi kuhusishwa na mauaji haya,bado upelelezi unaendelea
 

ASKOFU DKT NDALIMA AWATAKA VIONGOZI WA DINI KUZIDI KUMUOMBEA RAIS DKT MAGUFULI AWAONYA WANAOGEUZA MAKANISA MAJUKWAA YA SIASA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Askofu  wa  kanisa la Pentecote Tumaini Gospel Centre nchini Tanzania  Dkt  Rejoice Ndalima akifaya maombi
Baadhi ya  waumini  wa kanisa hilo
mchungaji Kiongozi wa kanisa hilo Iringa Paul Mtakwimwa
Askofu  wa kanisa la Pentecoste Tumaini Gospel Centre nchini Tanzania  Dkt  Rejoice Ndalimaakiwaombea  waumini wake na Taifa
Wachungaji wakiwa katika maombi
Askofu  wa kanisa la Pentecoste Tumaini Gospel Centre nchini Tanzania  Dkt  Rejoice Ndalima akimsimika mchungaji Paul Mtakimwa na mkewe
Waumini  wakiwa katika maombi maalum
Na MatukiodaimaBlog 
ASKOFU  mkuu  wa kanisa la Pentecote  Tumaini Gospel Centre nchini Tanzania  Dkt  Rejoice Ndalima  amewataka  viongozi wa  dini  nchini  kutumia nyumba  za ibada  kumwombea Rais Dkt John Magufuli na  kuliombea Taifa badala ya kutumia nyumba  hizo kusema kuumbua viongozi  wa  serikali .

Kuwa kazi kubwa inayofanywa na Rais Dkt Magufuli katika  nchi  hii si  ya kubenzwa makanisani na wachunguzaji ama viongozi wengine wa  dini bali ni kazi ambayo inapaswa  kuombewa  zaidi  ili  Taifa  lizidi kubarikiwa .

Askofu  huyo ametoa kauli hiyo jana  wakati wa  uzinduzi wa kanisa hilo  Mtwivila  mjini Iringa pamoja na kumsimika mchungaji kiongozi wa kanisa hilo Paul Mtakwimwa   ,kuwa hivi  sasa  heshima ya  nyumba  za ibada  imeanza kupoteza uwepo  wa Mungu kutokana na baadhi ya  watu  kutumia  nyumba   za  ibada kama  sehemu ya masengenyo na utapeli jambo  ambalo  si  sahihi .

Alisema  kitendo  cha baadhi ya makanisa nchini kutumiwa na wanasiasa ama vikundi vya  watu  kuishambulia serikali ama  kufanya utapeli  wa fedha  za  waumini wao kwa kuwatoza fedha  kama malipo ya huduma  wanayoitoa si  sahihi na si kazi ya  nyumba  za ibada hasa makanisa .

Pasipo  kutaja majina ya makanisa   yaliyogeuzwa majukwaa ya wanasiasa na baadhi ya  watu  waovu ama yanayofanya utapeli  wa  pesa  kwa  waumini  wake ,alisema  kuwa yamezuka makanisa ambayo kimsingi hayakupaswa  kuitwa makanisa  ili yalipaswa kuwa ni vyama  vya siasa ama nyumba  za  waganga  wa  kienyeji kwa maana ya  wapiga ramli .

“ Baadhi ya makanisa  yamepoteza sifa ya  kuitwa ni makanisa maana  wanafanya  vituko vya ajabu sana  ndani ya madhabahu ya Mungu …wapo  wanaotumiwa na wanasiasa  kueneza siasa makanisani na  kila  siku  wao ni kuwa ni wachonganishi  dhidi ya  serikali na  watu wake na wengine wamegeuka  watabiri wa  uongo na watenda miujuzi hatarishi kwa jamii “

Alisema  kuwa kazi ya viongozi wa  dini  ni  kuhubiri  neon ili  watu  wote  waweze kumjua Mungu na  sio kuhubiri siasa ama  kuifundisha kazi serikali ya  kufanywa wakati si  jukumu la kanisa kuwa  iwapo watu  wote  watamjua  Mungu  watafanya kazi ya kuhudumia  jamii  kwa  kutanguliza  hofu ya  Mungu hivyo  hakutakuwa na ufisadi , wizi ama watumishi  hewa hivyo kazi ya kanisa ni kuwafanya watu waijue kweli na kweli  iwe ndani ya  mioyo yao.

Askofu Dkt   Ndalima  alisema kuwa kanisa   lake  limeenea  nchi nzima na katika mkoa  wa Iringa  wameanzisha makanisa mawili  katika  mji  wa Iringa na Nyololo  wilaya ya  Mufindi ila lengo lao ni  kuhubiri neon la Mungu kwa usahihi na kuepuka kuwa  kanisa la ujanja ujanja  kama  wanavyofanywa baadhi ya  watu  wanaojiita manabii  ila kazi wanayoifanya  ni  sawa na manabii  wa uongo .
Akielezea  kuhusu utendaji kazi wa Rais  Dkt  Magufuli askofu  huyo  alisema kanisa lake  linampongeza kwani hivi sasa nchi imekuwa na utulivu mkubwa na hakuna  tena maandamano ya  vurugu na  kuwa kila wakati makanisa  yake yatatenga mudu  wa  kumuombea Rais na  watendaji  wote wa serikali na kutumia Biblia katika ibada  zake na  sio  kutumia  matukio na kashfa  za  viongozi  kuhubiri kanisani .
MWISHO

KATIBU WA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) WILAYA YA MUFINDI JIMSON MHAGAMA AJITOSA UBUNGE WA AFRIKA MASHARIKI.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. code:
Katibu wa chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Mufindi Jimson Mhagama  akiwa kwenye mmoja ya mikutano ya kampeni wa kumtafuta diwani wa kata ya Igombavanu wilayani mufindi akikitumikia chama.
 Katibu wa chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Mufindi Jimson Mhagama  akiwa kwenye mmoja ya mikutano ya kampeni akimwombea kura Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Maguli mwaka 2015 katika uwanjwa wa wambi mafinga.
 Katibu wa chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Mufindi Jimson Mhagama  akipeana mkono na waziri mkuu mstaafu wa awamu ya nne mh Mizengo Pinda kwenye moja ya majukumu ya kukitumikia chama.
Katibu wa chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Mufindi Jimson Mhagama  akipeana mkono na Rais mstaafu wa awamu ya nne dr Jakaya Mrisho Kikwete na kubadilishana maneno ya hapa na pale

 Na Fredy Mgunda, Mufindi

KATIBU wa chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Mufindi Jimson Mhagama ametangaza nia ya kugombea nafsi ya kuchaguliwa kuwa mbunge wa bunge la afrika mashariki kwa kuiwakirisha Tanzania.

Akizungumza kwa njia ya simu Mhagama alisema kuwa atahakisha lugha ya kiswahili inatumika barani afrika kama lugha mama kwa kuwa ndio lugha ilisamba zaidi barani afrika.

“Nimetembea nchi nyingi hapa afrika nimekutana na watu wengi wanazungumza Kiswahili hivyo hoja yangu itakuwa kuahakikisha natimiza kitu alichotuachia hayati baba wa taifa mwalimu Julias Kabarage Nyerere”.alisema Mhagama

Mhagama alisema kuwa atalazimaka kuwatetea wakulima kwa kuwa asilimia kubwa ya watanzania wengi ni wakulima na uchumi wetu bado unategemea kilimo hivyo ni lazima kuwekeza nguvu kwenye kilimo chenye tija na kufanikiwa kuinua mazao yanayozalishwa hapa nchi na kukuza uchumi.

“Tanzania tumebatika kuwa na ardhi nzuri na kubwa ambayo kwa asilimia kubwa bado haijatumika kwa mjibu wa wataalam wa kilimo hivyo ni lazima kutafuta nja mbadala ya kuwainua wakulima hawa ili kuviwezesha viwanda vyetu kupata mali ghafi nyingi na za kutosha ili kuinua kipato cha kila sekta hapa nchi”.alisema Mhagama

Aidha Mhagama amewataka watanzania kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli kwa kazi anazozifanya kwa kutafuta njia bora ya kuinua uchumi wa wananchi wake kutoka hapaulipo hadi kufikia uchumi wa viwanda kama sera yake alivyoielekeza kwenye Tanzania ya viwanda.

“Angalia sasa tunapata wawekezaji wengi kwenye sekta ya viwanda hii ni dalili nzuri ya kuukalibia uchumi wa viwanda hivyo nikiwa mbunge wa bunge la Afrika Mashariki nitandelea kuunga mkono Rais kwa kutafuta njia za kuwanua wawekezaji wazawa ili waboreshe na kuanzisha viwanda vyao”.alisema Mhagama

Mhagama aliwaomba watanzania kwa ujumla kumuombea ashinde kiti hicho ili aweze kuiwakirisha vyema nchi kwa uadilifu uliotukuka
 
Powered by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Iringa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa