Home » » WAZIRI MKUU MHE. KASSIM MAJALIWA ATAKA UJENZI WA HOSPITALI YA MJI MAFINGA UKAMILIKE KWA WAKATI

WAZIRI MKUU MHE. KASSIM MAJALIWA ATAKA UJENZI WA HOSPITALI YA MJI MAFINGA UKAMILIKE KWA WAKATI

“TUNATAKA NDUGU ZETU AMBAO NI WAGONJWA MAHUTUTI KUTOKA MAFINGA WAHUDUMIWE HAPA HAPA KATIKA HOSPITALI YA MJI MAFINGA KWENYE JENGO LA WAGONJWA WANAOHITAJI UANGALIZI MAALUMU( ICU) BADALA YA KUWAKIMBIZA NA GARI LA WAGONJWA KUWAPELEKA KUPATA HUDUMA HOSPITALI NYINGINE, HUDUMA ZA ICU ZITAPATIKA HAPA , HIVYO MALIZENI UJENZI HUU HARAKA , ILI WANANCHI WAPATE HUDUMA HII”

Kauli hiyo imetolewa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa( MB)  alipofanya ziara Wilaya ya Mufindi katika Hospitali ya Mji Mafinga iliyopo katika Halmashauri ya Mji Mafinga.

Waziri Mkuu amesema kiu ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kuona wananchi wanapata huduma safi, bora na haraka katika maeneo waliyopo  bila kusafiri umbali mrefu kupata huduma huko, ndio maana  Serikali imeleta kiasi cha shilingi Milioni 900 ili kujenga Miundombinu katika Hospitali hii ya Mji Mafinga.

“Serikali Kuu kupitia Rais wake Dkt. Samia Suluhu Hassan inajali wananchi wake, ndio maana fedha hizi zimekuja hapa Halmashauri ya Mji Mafinga, lengo ni kuona wananchi wanapata huduma bora. Niwaagize ifikapo tarehe 1/8/2024 hakikisheni majengo haya yanatoa huduma, kamilisheni haraka, lipeni mafundi kwa wakati ili wafanye kazi kwa moyo”

Akitoa taarifa ya Ujenzi wa Miundombinu katika Hospitali ya Mji Mafinga, Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji Mafinga Dkt . Bonaventura Chitopella amesema, majengo yanayojengwa baada ya kupokea fedha Milioni 900 ni Jengo la Wagonjwa wanaohitaji Uangalizi Maalumu( ICU), Jengo la Mama na Mtoto yaani Maternity Complex na Jengo la kufulia .
Amesema majengo yote yamekamilika kwa asilimia 85 na yakikamilika huduma zote muhimu na bora zitatolewa katika Hospitali ya Mji Mafinga.

Aidha Waziri Mkuu Mheahimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa(Mb) amepongeza Baraza la waheshimiwa Madiwani, Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mufindi pamoja na Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Mafinga kwa usimamizi mzuri wa Ujenzi wa Miradi hii mikubwa na ameomba ikikamilika basi huduma zianze kutolewa mapema.

Imeandaliwa na Kitengo cha Mawasiliano Swrikalini- Mafinga TC

Sima Mark Bingileki
Mkuu wa Kitengo Cha Mawasiliano- Mafinga TC



0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Iringa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa