Kamati ya Uchumi, Elimu na Afya ya Halmashauri ya Mji Mafinga Imefanya ziara kukagua Mradi wa Ukamishaji wa Mabweni Mawili ya wasichana katika Shule ya Sekondari Changarawe iliyopokea Shilingi Milioni 67.7 kutoka Serikali Kuu kwaajili ya Ukamilishaji wa mabweni mawili.
Akitoa taarifa kwa Kamati hiyo Mkuu wa Shule ya Changarawe Mwalimu Peter Mbata amesema Halmashauri ya Mji Mafinga kupitia Shule ya Sekondari Changarawe ilipokea fedha kutoka Serikali kuu kwaajili ya Ukamilishaji wa Mabweni hayo mawili.
Amesema ukamilishaji huo umehusisha upakaji wa Rangi, uwekaji wa malumalu,utengenezaji wa Mifumo ya Maji na ukamilishaji unatarajia kukamila tarehe 14/7/2024. Mabweni hayo yanatumiwa na wanafunzi wa kike 240.
Wajumbe wameshauri ukamilishaji uende kwa haraka ili kuwaruhusu wanafunzi kuanza masomo kwani kwa kuwa na miundombinu bora shuleni inachochea kuongeza mori kwa wanafunzi kusoma.
Shule ya Sekondari Changarawe ina jumla ya wanafunzi 1284 na Inapatikana katika Halmashauri ya Mji Mafinga.
Sima Bingileki
Mkuu wa Kitengo Cha Mawasiliano Serikalini
0 comments:
Post a Comment