Home » » SASA REDD'S MISS IRINGA JUNI 20

SASA REDD'S MISS IRINGA JUNI 20

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

HATIMAYE kinyang’anyiro cha kumsaka Redd’s Miss Iringa kinatarajia kufanyika Juni 20, baada ya aliyekuwa Mratibu wa kwanza, Mohamed Mcholeka kutoweka katika mazingira ya kutatanisha na kushindwa kufanyika Juni 6 kama lilivyokuwa imepangwa.
Hivi karibuni, Tanzania Daima iliripoti kutoweka kwa Mcholeka katika mazingira ya kutatanisha, huku wadau wa urembo wakiwataka waratibu wa Miss Tanzania, Kampuni ya Lino Agency chini ya Hashim Lundenga ‘Uncle’ kumchukulia hatua na kuliokoa shindano hilo.
Lino Agency baaada ya kugundua hilo, wamempa kibali cha kuandaa shindano hilo ambalo lilikuwa linasubiriwa kwa hamu kubwa na wadau wa tasnia ya urembo, Kampuni ya Chakudika Entertainment chini ya uongozi wake, Victor Chakudika, ambaye ni meneja wa kituo cha redio cha Nuru Fm cha mjini hapa.
Akizungumza na Tanzania Daima ofisini kwake jana, Chakudika alisema uamuzi wa kuchukua jukumu hilo kwa sasa, umelenga kutopoteza vipaji vya mabinti waliokuwa tayari kushiriki shindano hilo na kuondoa aibu ya Mkoa wa Iringa kutopeleka mwakilishi katika shindano la Redd’s Miss Nyanda za Juu, ambako wamekuwa wakishiriki kila mwaka.
Alisema kuwa shindano la Redd’s Miss Iringa limekuwa chachu ya ajira kwa mabinti wengi mkoani hapa, kwa kuweza kutangaza vipaji vya washiriki wanaojitokeza kushiriki kila mwaka.
Chakudika alisema shindano hilo linatarajiwa kuwa la kisasa kutokana na maandalizi yake kuendelea vema na kuwataka wadau wa tasnia ya urembo, kujitokeza kwa wingi katika Ukumbi wa St. Dominic litakapofanyika shindano hilo.
Aliongeza kuwa hadi sasa warembo 12 wamejitokeza kushiriki shindano hilo na wanaendelea na mazoezi katika Ukumbi wa Hoteli ya Gentle Hill mjini hapa na msanii Mo Music anayetamba na wimbo ‘Basi Nenda’ anatarajia kutoa burudani kali katika shindano hilo, sambamba na wasanii wengine chupukizi wa mjini Iringa, vikundi vya sanaa na ‘Wakali wa Kudance’ wa mjini Iringa.
Mbali na Redd’s, wadhamini wengine ni Nuru Fm, kampuni mpya ya mabasi ya Sutco High Class na Gentle Hills.
Chanzo;Tanzania Daima 

0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Iringa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa