Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
MBUNGE wa Arusha Mjini, Godbless Lema, amesema Tanzania inatia aibu
kwa kugeuka ombamba huku ikiwa na rasilimali nyingi ambazo
zinawafaidisha wachache wasiona uchungu na nchi.
Lema, alitoa kauli hiyo hayo juzi alipowahutubia wakazi wa Kata ya
Miyomboni-Kitanzini katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja
wa Mnada (Well Fair) katika Manispaa ya Iringa.
Alisema watu wanaoiba rasilimali za nchini wanalindwa kama dhahabu huku masikini wakibambikiziwa kesi za ajabu ajabu.
“Ndugu zangu, tunapopambana na CCM, tunapambana na wezi, majambazi,
mafisadi, wahuni na mafilauni. Unapokuwa na chama kinachouza ndovu,
madini, misitu, na ardhi, uhusiano wao na shetani ni wa karibu.
“Unapokuwa na chama kinachotoa sukari kiwandani kwa sh 1,000 na
kutoza kodi hadi kufikia 2,000 au ukiwa na chama ambacho saruji
kiwandani inatengenezwa kwa sh 4,000 na kutoza kodi hadi kufikia sh
15,000 ni chama cha mauaji,” alisema Lema.
Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa, alisema ikiwa nchi
yenye rasilimali nyingi kama Tanzania inategemea asilimia 40 ya bajeti
znima kutoka kwa wahisani na wafadhili mbalimbali, nchi haina viongozi
wenye uwezo wa kufiki jinsi ya kujitegemea.
Alisema cha kushangaza kuna wabunge ambao wapo madarakani kwa miaka
mingi, lakini majimbo yao hayana maendeleo kwa muda mrefu. lakini kazi
yao ni kuunga mkono bajeti hewa.
“Mipango yote inaandaliwa kwa ajili ya matajiri na makampuni makubwa
yanayokweta kulipa kodi pamoja na kuiba rasilimali za umma au kuwaibia
Watanzania” alisema.
Alisema inapoonekana mmoja anaonewa, jamii inapaswa kupiga kelele kwa kuwa kuonewa kwa mtu mmoja ni kuonewa kwa jamii nzima.
“Akionewa machinga, nesi hapaswi kukaa kimya, akionewa mwalimu
machinga hapaswi kukaa kimya. Watu wote tunategemeana kwa kazi
tunazozifanya” alisema.
Chanzo;Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment