Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
MFUKO
wa Hifadhi ya Misitu Tanzania (TaFF) kwa kushirikiana na Mtandao wa
Jamii wa Usimamizi wa Misitu Kanda ya Kitapilimwa (MJUMIKK) umewakabidhi
wajasiriamali mashine sita za kukamua asali na mizinga 20.
Vifaa kazi hivyo vilipokelewa na vikundi vya ujasiriamali vinavyorina asali kata za Kitapilimwa na Kiwele, Ismani mkoani Iringa.
Akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano iliyofanyika katika
Kijiji cha Kinywang’anga hivi karibuni, Katibu wa mtandano wa MJUMIKK,
Samson Fuko, alisema lengo ni kuleta ufanisi wa kulinda, kutunza na
kutumia kwa njia endelevu rasilimali za misitu na kuongeza kipato cha
mjasiriamali.
Alisema mashine hizo zitakuwa shamba darasa la ufugaji wa nyuki na
upandaji miti utakaotoa mafunzo ya vitendo kwa wanachama wake na elimu
kwa jamii juu ya uhifadhi wa mazingira.
Fuko alisema mtandao huo umefanikiwa kuongeza idadi ya wanachama
kutoka 50 waliokuwepo awali hadi 200 waliopo sasa ambao wanajihusisha na
ufugaji wa nyuki unaotekelezwa katika vijiji sita kati ya 11 vya
Ismani.
Alivitaja vikundi vilivyofaidika na msaada huo kuwa ni Kinywang’anga,
Faraja Group, Twiga Group, Mshikamano, Jitegemee na Umoja,
vilivyopatiwa mizinga, mashine, zana za kukamulia asali na mavazi
maalumu ya kurinia asali vyenye thamani ya sh milioni 4.5.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa, Jesca
Msambatavangu, aliyeshuhudia makabidhiano hayo, aliwaasa wazazi na
walezi kuwahamasisha vijana wao wajiunge kwenye shughuli za maendeleo.
Chanzo:Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment