Home » » MBUNGE MGIMWA AANZA KUTIMIZA AHADI ZA MAREHEMU BABAKE KWA KASI KUBWA

MBUNGE MGIMWA AANZA KUTIMIZA AHADI ZA MAREHEMU BABAKE KWA KASI KUBWA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

‘Hongera sana mheshimiwa kweli umeanza kwa mfano “ 
Katibu mwenezi wa CCM wilaya ya Iringa Denis Lupala kulia akimpongeza diwani wa kata ya Nzihi kwa kazi nzuri 
Wananchi wa Ilala Simba wakimsikiliza mbunge Mgimwa 
Uongozi wa kijiji cha Ilala Simba ukimkabidhi mbunge Mgimwa risala yao 
Mbunge Mgimwa akikabidhi mipira kijiji cha Ilala Simba leo 
Sehemu ya saruji iliyotolewa leo na mbunge Mgimwa 
Mbunge wa jimbo la Kalenga Godfrey Mgimwa akiwahutubia wakazi wa kijiji cha Nyamihuu katika ziara yake ya kuwashukuru na kupokea changamoto mbali mbali 
Mmoja kati ya wazee walemavu kijiji cha Nyamihuu kalenga akimwomba mbunge Mgimwa msaada wa baiskeli ya walemavu 
Kiongozi wa serikali ya kijiji cha Nyamihuu akipokea mipira kwa ajili ya kuendeleza michezo kwa vijana 
Wazee kijiji cha Nyamihuu wakimpa baraka na kumpongeza mbunge Mgimwa kwa uchapa kazi wake 
Bw Kiswaga akimpongeza mbunge Mgimwa kwa kuonyesha usikivu mkubwa kwa wananchi 

MBUNGE wa jimbo la Kalenga mkoani Iringa Godfrey Mgimwa ameanza kutimiza ahadi zake kwa wananchi wa jimbo la kalenga kwa kukabidhi mifuko zaidi ya 150 ya saruji katika kijiji cha Magubike na kijiji cha Kidamali kata ya Nzihi yenye thamani ya zaidi ya Tsh milioni 2.5

Saruji hiyo mifuko 100 kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa jengo la utawala shule ya sekondari Dimitrios katika kijiji cha Magubike na mifuko 50 kwa ajili ya shule ya sekondari Kidamali.

Mgimwa alisema kuwa lengo la kutimiza ahadi yake hiyo ni kama njia ya kuwashukuru wana Kalenga kwa kumchagua katika uchaguzi mdogo uliofanyika hivi karibuni pia kutimiza ahadi mbali mbali binafsi ambazo alizitoa mbunge aliyefariki marehemu Dr Wiliam Mgimwa.

Alisema ataendelea kutimiza ahadi binafsi zilizotolewa na marehemu Dr Mgimwa kulingana na uwezo wake na zile za kitaifa ambazo zipo katika Ilani ya CCM atahakikisha anaikumbusha serikali ya CCM ili kutimiza ahadi hizo kwa wakati.

“Ndugu zangu wananchi mbali ya kuwa ubunge wangu ni wa mwaka mmoja ila tayari mimeanza kutimiza ahadi bila ya kuchelewa na ninawahakikishieni sita waangusha nitaendelea kufanya hivyo zaidi mniombee uzima”

Alitaja maeneo ambayo tayari amekabidhi ahadi zilizotolewa na mbunge aliyefariki kuwa ni pamoja na Kiwere shule ya msingi mifuko 80 ya saruji,shule ya msingi wangama bati 100 na saruji mifuko 50,shule ya msingi Negabii bati 100 ,shule ya msingi Mibikimitali bati 50 ,Kijiji cha Isupilo bati 50 na saruji mifuko 50 na maeneo mingine mengi.

Pia amekabidhi kiasi cha Tsh 500,000 kwa ajili ya kuchangia kuwezesha kusajili timu ya kata ya Nzihi na nyingine kwa ajili ya ukarabati wa soko

0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Iringa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa