Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
CHAMA cha Soka Mkoa wa Iringa (Irefa), kwa kushirikiana Shirikisho
la Soka Tanzania (TFF), na Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA),
wanatarajiwa kujenga uwanja wa kisasa katika eneo la Kitwiru mkoani
hapa.
Hayo yalibainishwa juzi, wakati aliyekuwa Katibu Mkuu wa Irefa,
Eliud Mvela ‘Wamahanji’ ambaye kwa sasa ni Mkurugenzi Msaidizi wa
Sheria na Uanachama wa TFF, wakati akizungumza na waandishi wa habari
katika ukumbi wa hoteli ya Embalasasa, kwa lengo la kuwaaga na kutoa
shukrani kwa ushirikiano kipindi cha uongozi wake.
Alisema, wanatarajia kujenga Uwanja huo, ambao utakuwa chini ya
Baraza la Wadhamini, hivyo kuruhusu michezo mikubwa kufanyika na
kuongeza hamasa kwa vijana kujiajiri kupitia sekta ya michezo.
“Moja ya mafanikio ambayo nitayaacha ni jitihada za kuanza makakati
wa ujenzi wa uwanja wa kisasa wa nyasi bandia katika Manispaa ya
Iringa, utakaojengwa eneo la Kitwiru chini ya ufadhili wa FIFA na TFF
na kuwa, jitihada za ujenzi zinaendelea kufanyika na Manispaa ya Iringa
tayari imetoa eneo,” alisema Wamahanji.
Wamahanji alisema, mchakato wa kuujenga uwanja huo umeanza na barua
ya kukubaliwa imeshatoka na utakuwa moja ya viwanja vitano bora
Tanzania, hivyo kusaidia kukuza soka la Mkoa wa Iringa.
Aliongeza kuwa, katika uongozi wake mengi amefanya, ikiwemo kuacha
timu mbili zinazoshiriki ligi daraja la kwanza na kuondoa migogoro
ndani ya chama ambayo ilikuwepo hapo kabla.
Chanzo:Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment