Mkuu
wa mkoa wa Iringa Dkt.Christina Ishengoma amewapongeza wananchi wa mkoa
huo kwa ushirikiano wao katika shughuli za kujiletea maendeleo ya
kiuchumi na kijamii.
Akizungumza
na waandishi wa habari ofisini kwake Dkt.Christina Ishengoma amesema
katika kipindi cha mwaka 2013 wananchi wa mkoa wa Iringa wamekuwa
wakifanyakazi kwa kujituma na kwa ushirikiano mkubwa.
Kwa
upande mwingine ishengoma amewataka wananchi wote wa mkoa wa
iringa kuzitumia mvua zinazoendelea kunyesha kwa sasa kupanda mazao
yanayovumilia ukame ambayo ni Mtama, Muhogo, Viazi vitamu na Ulezi kwa
na kila familia ihakikishe inapanda chini ya hekari mbili.
Amesema kuwa kwa kufanya hivyo kutawahakikishia uhakika wa chakula hasa maeneo ambayo hupata mvua chache. Hata
hivyo mkuu wa mkoa huyo amewaasa wananchi kutumia mbegu bora za
kilimo,mbolea ya kundia na kukuzia hasa kwa mazao ya mahindi na mpunga
ili kupata mazao bora.
Aidha
Ishengoma amewatakia heri ya krismasi na mwaka mpya huku akiwahakikishia
kuimalishwa kwa ulinzi katika kipindi hiki cha sikukuu.
0 comments:
Post a Comment