Kanali
Mjengwa akisalimiana na naibu katibu mkuu CCM Bara Mgulu Nchemba leo
nje ya kanisa la RC Rujewa baada ya kukutana kwa shughuli za mazishi ya
aliyekuwa katibu wa CCM mkoa wa Iringa Emanuel Mteming'ombe
Na Francis Godwin Blog
MWENYEKITI
wa Chama cha mapinduzi (CCM) Taifa Dr Jakaya Mrisho Kikwete
ametuma salam za rambirambi kwa uongozi wa CCM mkoa wa Iringa na
familia ya aliyekuwa katibu wa CCM mkoa wa Iringa Emanuel
Mteming'ombe aliyefariki dunia juzi na kuzikwa leo katika
mji wa Rujewa Mbarali mkoani Mbeya.
Salam
hizo za Rais Dr Kikwete zilitolewa jana wakati wa mazishi ya
Mteming'ombe na naibu katibu mkuu CCM Bara Bw Mwinhulu Nchemba
ambae alikiwakilisha chama taifa katika mazishi hayo .
Alisema
kuwa Rais Dr
Kikwete ambae yupo nchini Marekani kwa ziara za kiofisi amepokea
kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha katibu huyo na kuwa
alitamani sana kuweza kufika Rujewa mkoani Mbeya kwa ajili ya
kushirikia mazishi hayo ila ameshindwa .
"
Nitoe salama za aina tatu salama ya kwanza kutoka kwa mheshimiwa
Rais Dr Kikwete akiwa mwenyekiti wetu wa Chama taifa amepokea kwa
masikitiko makubwa taarifa hii ya kifo na wakati
anapata taarifa hii tayari alikuwa katika ndege kuelekea nchini
Marekani .....kama tunavyojua Rais wetu ni mwepesi kufika katika
misiba ila ameshindwa na kuniagiza mimi kutoa salam zake kwa niaba
yake"
Hata
hivyo alisema kuwa salama za pili ni kutoka kwa katibu mkuu wa CCM
Taifa ambapo amepokea kwa masikitiko makubwa zaidi kutokana na kifo
hicho kutokana na katibu huyo marehemu Mteming'ombe enzi za uhai
wake alikuwa msaada mkubwa sana kwa chama kutokana na kuwa mwepesi
zaidi.
Alisema kuwa wao kama chama wataendelea kuwa karibu na familia ya marehemu ikiwa ni pamoja na kuitunza familia hiyo.
Kwa
upande wake mkuu wa mkoa wa Iringa Dr Christine Ishengoma akitoa
salama za serikali mkoa wa Iringa kufuatia kifo hicho alisema kuwa
katika kipindi hiki cha maombolezo na baada ya maombolezo viongozi
wa chama na serikali mkoa wa Iringa hawana budi kuendelea kufanya
kazi kwa kushirikiana zaidi kama njia ya kumuenzi Mteming'ombe.
Huku
mkuu wa
mkoa wa Mbeya Abas Kandoro akisisitiza viongozi wa umma na chama
kujenga utamaduni wa kushirikiana na kuacha tabia ya kujitenga na
jamii.
Wakati
huo huo waombolezaji waliofulika makaburini hapo walionyesha
kushindwa kujizuia kushangilia kwa furaha kubwa wakati mwenyekiti wa
CCM mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu akisoma mchango wa waziri
mkuu aliyejiuzulu Edward Lowasa mchango wa Tsh milioni 1 alioutuma kwa
uongozi wa CCM mkoa wa Iringa kwa
ajili ya shughuli za mazishi ya Kiongozi huyo.
Katika
tukio jingine vijana wanaosadikika kuwa na wafuasi wa Chadema
wakiwa na sare za chama hicho wamejikuta wakichezea kichapo kutoka
kwa vijana wa UVCCM baada ya kuwavamia vijana hao katika kanteni ya
polisi Rujewa ambako walikuwa wakijipumzisha kwa uchovu .
Imedaiwa
kuwa vijana wapatao wanne walifika eneo hilo na kuanzisha vurugu
hali iliyopelekea vijana wa UVCCM kutoka mkoa wa Iringa na Mbeya
kuwafunza adabu na polisi kuwakamata vijana hao wa Chadema na
kuwatupa mahabusu.
Mwenyekiti
wa UVCCM mkoa wa Iringa Tumain Msowoya alisema amezipata habari hizo
japo alisema kuwa hakuna majeraha makubwa yaliyowapata vijana wa CCM
mbali ya wavamizi hao kuwa shambulia kwa chupa .
AWALI AKISOMA WASIFU
WA MAREHEMU EMMANUEL MTEMING’OMBE ,MWENYEKITI WA CCM MKOA WA IRINGA JESCA MSAMBATAVANGU ALISEMA
Marehemu
Emmanuel Mteming’ombe alizaliwa tarehe 25/ 06/ 1956 katika kijiji cha Rujewa, Wilaya
ya Mbarali, Mkoa wa Mbeya.
2.
ELIMU NA MAFUNZO.
Marehemu
Emmanuel Mteming’ombe alipata elimu yake ya msingi katika shule ya msingi
Chimala, Mbeya kati ya mwaka 1972 – 1978. Baada ya kumaliza darasa la saba,
marehemu alijiunga na masoma ya sekondari katika shule ya sekondari ya wavulana
Songea kuanzia mwaka 1979 – 1982.
Kati
ya mwaka 1986 -1989 marehemu alijiunga na Chuo cha Uganga Songea akisomea kozi
ya Utabibu.
3.
UTUMISHI WA SERIKALI.
Mwaka
1991, marehemu aliajiriwa serikalini kwa cheo cha Medical Assistant (Tabibu),
kazi aliyofanya kwa miaka mnne hadi mwaka 1994 alipoamua kuacha kazi na
kufungua Duka la Dawa na Zahanati yake binafsi.
4.
UTUMISHI KATIKA CHAMA CHA MAPINDUZI.
Nyota
njema huonekana asubuhi. Marehemu Emmanuel Mteming’ombe akiwa Chuo cha Utabibu Songea
kati ya mwaka 1986 – 1989 alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa Umoja wa vijana Tawi
kwa muda wote aliokuwa Chuoni hapo.
Mara
baada ya kumaliza masomo yake ya Utabibu alipata tena nafasi ya kuchaguliwa
kuwa Mwenyekiti wa UVCCM wa kata ya Rujewa, Mbarali kuanzia mwaka 1990 – 1994.
Kutokana na uhodari aliouonesha, marehemu mwaka 1994 alichaguliwa kuwa
Mwenyekiti wa kijiji cha Rujewa hadi mwaka 1999.
Mwaka
1998, Marehemu Emmanuel Mteming’ombe alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa
wa Mbeya, nafasi aliyoshika hadi mwaka 2003. Katika uchaguzi Mkuu wa Serikali
wa mwaka 2000,Marehemu alichaguliwa kuwa Diwani wa kata ya Rujewa, nafasi
aliyoshika hadi octoba, mwaka 2005.
Kutokana
na uwezo wake mkubwa wa Uongozi aliouonesha katika nafasi mbalimbali za
uongozi, Sekretarieti ya Halmashauri Kuu
ya Taifa ya CCM iliyokutana tarehe
26 – 27/ 03/ 2003 ilimteua kuwa Kaimu
Katibu wa CCM wa Wilaya na kupangiwa kwenda kufanya kazi katika wilaya ya
Kyela. Baada ya kuonekana anamudu nafasi ya Katibu wa CCM wa Wilaya, Kamati Kuu ya Halmashauri
Kuu ya CCM ya Taifa iliyokutana tarehe 19 -20/ 03 2004 ilimthibitisha kuwa Katibu wa CCM wa Wilaya.
Marehemu
Emmanuel Mteming’ombe, akiwa Katibu wa CCM wa Wilaya alifanya kazi katika
Wilaya za Kyela, Ireje, Mbozi ambako alionyesha uwezo mkubwa wa Uongozi na kuwa
tegemeo la Chama Cha Mapinduzi.
Marehemu
Emmanuel Mteming’ombe aliteuliwa kuwa Kaimu
Katibu Wa CCM wa Mkoa wa Mbeya,
kuanzia tarehe 29/ 01/ 2008 na baadaye kuwa Katibu wa Mkoa na kumpangia kwenda
katika Mkoa wa Ruvuma ambako alifanya kazi hadi tarehe 28/ 05/ 2012
alipohamishiwa Mkoa wa Iringa.
5.
UGONJWA.
Marehemu
Emmanuel Mteming’ombe alianza kuumwa tarehe 02/ 12/ 2013 akieleza kuwa baada ya
kuonana na Daktari iligundulika kwamba anasumbuliwa na homa ya Matumbo
(Typhoid), Athma na Figo yake ya upande wa kushoto ikaonekana kuwa ina matatizo
na kupewa dawa ambapo alirejea nyumbani kwake na kuendelea kutumia.
Ilipofika
tarehe 17/ 12/ 2013 usiku, Marehemu alizidiwa na kupelekwa Hospitali Kuu ya
Mkoa wa Iringa ambapo madaktari walijitahidi kumhudumia, lakini ilipofika saa 8
usiku wa tarehe 19/ 12/ 2012 alifariki Dunia.
Marehemu
ameacha Mjane na Watoto Watatu.
Bwana alitoa na Bwana ametwaa Jina
la Bwana Lihimidiwe
Amen.
|
0 comments:
Post a Comment