WASOMII
wa vyuo vikuu kote nchini wameshauriwa kujiunga na vyuo vya mafunzo
ya ufundi Stadi "VETA", ili kujiongezea ujuzi na maarifa ya kufanya
kazi, kwa lengo la kujiajiri wenyewe katika sekta binafsi, hatua ambayo
itapunguza utegemezi wa ajira serikalini.
Wito
huo umetolewa na mkuu wa Mkoa wa Iringa Dr. Christin Ishengoma, wakati
akifungua mkutano wa wakuu wa vyuo vya ufundi VETA, vilivyopo katika
mikoa ya Kusini, mkutano uliolenga kupeana mikakati juu ya utaratibu wa
uendeshaji wa vyuo katika mfumo mpya wa Compitance Base Assesment (CBI) -
mkutano uliyofanyika katika chuo cha ufundi cha Donbosco cha Manispaa
ya Iringa.
Dr.
Ishengoma amesema pia wazazio na walezi wanapaswa kuachana na dhana potofu ya
kuwa vyuo vya Veta vipo kwa ajili ya wasio na elimu pekee, huku akiitaka
kuwapeleka vijana wao katika vyuo hivyo vya ufundi vilivyosajiliwa, na kuwataka
wakuu wa vyuo kuajiri walimu wenye sifa.
Mkurugenzi wa vyuo
vya Veta Nyanda za juu kusini Monica Mbelle amesema Kanda ya kusini ina jumla
ya vyuo vya veta 74, huku mkoa wa Iringa ukiwa na vyuo 29, mkoa wa Njombe vyuo
23 Ruvuma pamoja na mkoa wa Ruvuma 22.
Bi.
Mbelle amesema katika msimu wa mwaka 2013/ 14 Veta inampango wa kujenga vyuo
vya Veta katika wilaya ya Ludewa, Chuo cha Wilaya ya Namtumbo pamoja na ujenzi
wa chuo cha Mkoa wa Njombe.
0 comments:
Post a Comment