LICHA ya mkoa
wa Iringa kuwa ni kati ya mikoa sita inayotegemewa kwa chakula kitaifa, bado
mkoa huo unakabiliwa na tatizo la ugonjwa wa Utapiamlo, ugonjwa unaotokana na
mlo duni, jambo ambalo linadhihilisha kutokuwepo kwa elimu ya lishe kamili.
Hayo
yamezungumzwa na mkuu wa mkoa huo wa Iringa Dr. Christine Ishengoma, wakati wa
uzinduzi wa ghara la mbolea ya Yara, eneo la Ipogolo mjini Iringa, ambapo mkuu
huyo amesema tatizo la lutapiamlo linawaathiri zaidi
wajawazito, watoto pamoja na wazee.
Dk. Ishengoma
amesema mkoa huo wa Iringa umeshika nafasi ya tatu kati ya mikoa inayokabiliwa
na ugonjwa wa Utapiamlo, nafasi ya kwanza ikishikiliwa na mkoa wa Dodoma mkoa
ambao unakabiliwa na changamoto ya uhaba wa mvua.
Aidha mkuu huyo
wa mkoa amesema ugonjwa wa utapiamlo kwa watoto walio na umri chini ya miaka
mitano mkoa wa Iringa unashika nafasi ya tatu kitaifa kwa asilimia 52, na kuwa
hiyo ni aibu kubwa kwa mkoa kutokana na Iringa kuwa na vyakula vya kutosha.
Dk. Ishengoma
amesema kitaifa, mkoa wa Dodoma unaongoza kwa kuwa na Utapiamlo mkali kwa
asilimia 56, huku ukifuatiwa na mkoa wa Lindi wenye asilimia 54, huku akiwaasa
mawakala kuacha tabia ya kutochezea vocha za ruzuku ya pembejeo za kilimo kwa
madai kuwa hali hiyo inawakwamisha wakulima.
Hata hivyo
ofisa biashara wa kampuni ya Yara Hilary Pato amesema lengo la kampuni ya yara
kusogeza huduma mkoani Iringa ni kuwasaidia wakulima kufikia malengo ya kilimo
chenye tija kwa kupata pembejeo kwa wakati unaofaa.
0 comments:
Post a Comment