Mwenyekiti wa MANET Bw Zuberi Mwachura kulia akieleza mkakati wa kupambana na vitendo vya ujangili katika hifadhi ya Taifa ya Ruaha leo |
Mbunge wa jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa akifafanua jambo |
Mgeni rasmi katika warsha ya siku moja ya kujadili vitendo vya ujangili katika hifadhi ya Taifa ya Ruaha Mbunge wa jimbo la Iringa mchungaji Peter Msigwa ( wa pili kushoto) akiwa na viongozi mbali mbali akiwemo mwenyekiti wa taasisi iliyoandaa warsha hiyo MANET Bw Zuberi Mwachura na viongozi wengine.
.............................. .............................. ........
Na Francis Godwin Blog, Iringa
MBUNGE wa jimbo la Iringa mjini kupitia chama cha Demokrasia na maendeleo (chadema)amempongeza Rais Jakaya Kikwete kwa mkakati wake wa kunusuru vitendo vya ujangili katika hifadhi za Taifa.
Huku mbunge huyo akidai kuwa anawajua viongozi mbali mbali na watu maarufu ambao wanaendelea kuendesha vitendo vya ujangili katika hifadhi ya Ruaha Iringa ikiwa ni pamoja na kulitumia gari la wagonjwa (Ambulence) kusafirisha meno ya tembo na atawataja wahusika bungeni.
Msigwa ambae ni waziri kivuli wa wizara ya maliasili na utalii alitoa pongezi hizo leo mjini Iringa wakati wakati akifungua kikao cha kujadili vitendo vya ujangili katika hifadhi ya Taifa ya Ruaha Iringa iliyoandaliwa na taasisi isiyo ya kiserikali ya Mazingira Netwark Tanzania (MANET).
"Awali ya yote napenda kumshukuru sana Rais Jakaya Kikwete kwa kuja na mikakati ya kweli ya kupambana na vitendo vya ujangili nchini kwa kutumia askari wa jeshi la lawanchi Tanzania (JWTZ)...huu ni mkakati mzuri ambao binafsi nimempongeza sana kwa hatua hiyo" alisema Msigwa
Kuwa ni mara kadhaa watanzania wamepata kusikia viongozi wa Serikali wenye dhamana wakisema kuwa mtandao wa majangili na wafanyabiashara haramu wa wanyamapori ni mpana na mgumu kuumaliza
Pia ni mara kadhaa pia Serikali imeendelea kukiri kuwa mtandao huu unawahusisha Wafanyabiashara wakubwa, Wanausalama, Wabunge, Wanasiasa na watu wenye dhamana ya uongozi katika taifa letu umekuwa ni kikwazo kikubwa katika vita dhidi ya ujangili.
“….Serikali imeendelea kutoa matamko kuwa itawataja wahusika wa biashara haramu dhidi ya wanyamapori na kuwachukulia hatua lakini cha kushangaza, mara zote hakuna hatua yoyote inayochukuliwa..ni jambo moja la msingi ambalo ningependa kulizungumza na kusisitiza hapa leo ni juu ya wajibu wa kila Mtanzania katika kuhakikisha kuwa tunaungana kwa pamoja katika vita dhidi ya biashara haramu ya wanyamapori”
Hivyo alisema hatua ya Rais Kikwete kuweka mkakati huo wa kutumia askari wa JWTZ katika kulinda hifadhi na kupambana na majangili ni jambo la kumpongeza.
Kwani alisema baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika tamko lake maarufu mwaka 1961 lijulikanalo kama Arusha Manifesto alisema yafuatayo:
“Uhai wa wanyamapori ni jambo muhimu na linalotuhusu sana sisi sote barani Afrika. Viumbe hawa wa porini, wakiwa katika mapori wanamoishi,sio muhimu tu kwa ajili ya kuajabiwa na kuvutia lakini pia ni sehemu ya maliasili yetu na pia ndio mustakabali wa maisha yetu ya baadaye”.
Alisema kuwa mwalimu Nyerere alitambua umuhimu wa kutunza wanyamapori kwa wakati huo tukiwa na hazina kubwa ya wanyama, lakini leo viongozi wa Serikali wameshikwa na kigugumizi katika kuhakikisha dira na jitihada za baba wa taifa letu ,vinatimizwa.
Hivyo alisema kama kiongozi ambaye wananchi wamenipa dhamana ya kuwawakilisha, nawiwa kutumia nafasi hiyo, kuendeleza juhudi zangu na kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha kuwa kila Mtanzania anakua mdau nambari moja wa kupinga biashara haramu ya wanyamapori kwani si tu kuwa inalitia hasara taifa letu bali pia inaweka hatarini maisha ya wanyamapori kwa vizazi vijavyo.
“Nachukua nafasi hii kuikumbusha na kuitaka Serikali kutimiza wajibu wake kwa kuwafikisha majangili na wafanyabiashara haramu wa wanyamapori katika vyombo vya dola na watendewe ipasavyo kwa mujibu wa Sheria”
Kuhusu watu maarufu mkoani Iringa wanaojihusisha na biashara ya pembe za ndovu na hata kutumia magari ya umma kama Ambulence kusafirisha pembe hizo za ndovu alisema kuwa ana idadi yao ndevu zaidi na kuwa katika kikao cha bunge kijacho ataweka hadharani majina yao.
0 comments:
Post a Comment