Na Gustav Chahe, Iringa
MBUNGE wa viti maalum
Chiku Abwao (CHADEMA) amesema wanawake nchini wamegeuzwa kuwa chambo ya watu
wabinafsi wasiopenda maendeleo ya watu wengine.
Abwao ametoa kauli hiyo
leo alipokuwa akiunda kikundi cha wanawake katika Mtaa wa Kinegamgosi Kata ya
Ruaha katika Manispaa ya Iringa ili kuwasaidia wanawake katika kujitegemea.
Akitoa elimu ya
ujasiriamali kwa wanawake hao amesema amefikia maamuzi hayo baada ya kuona akina
mama wengi wanakuwa wanyonge katika maendeleo na kutumia kama chambo kwa watu
waroho na wabinafsi nyakati za uchaguzi.
“Akina mama wengi
tumejifunga na kukata tama lakini tikisaidia na kupiga hatua mbele tunaweza
kujifungua. Wanawake wengi ndiyo wapiga kura waaminifu lakini tunatumika vibaya
na watu, tukishawawezesha kuingia madarakani wanakuwa hawana muda na sisi tena.
Tulikatae hilo” amesema.
Alisema umasikini
katika nchi hii si wa bahati mbaya bali unatengenezwa na watu ili waendelee
kuwepo madarakani kwa kugawa kofia, kanga na fulana wakati wa uchaguzi ili
waonekane wa maana zaidi kuliko wengune.
Pia amesema kuunda
vikundi vya akina mama na kuviwezesha ni utekelezaji wa mipango ya Chadema ili
kuwatengenezea mazingira mazuri ya maisha pamoja na uendeshaji wa familia zao.
“Umasikini wetu si wa
bahati mbaya kwa chama cha Mapindizi (CCM) bali ni makusudi yao. Wanatengeneza mazingira
ya umasikini ili wapate nafasi ya kuwarubuni watu. Tumekuwa kama kuku wa
kienyeji” amesma.
Alisema ili kuondokana
na umasikini ni lazima kuwa na dhamira ya kweli kuukataa ikiwa ni pamoja na
kuwakata wanaosababisha wengine kuishi kama watumwa.
Mwenyekiti wa kikundi
hicho Judith Muhali amesema umefika wakati wa kuachana na watu wanaotumia
majukwaa wa kati wa uchaguzi kwa kuwanunua wananchi ama kwa pesa ama kwa
kuwagawia vitenge au kofia kwa kuwa hivyo havileti maendeleo ba badala yake
amewataka akina mama kuungana na kufanya mambo ya maendeleo kwa kuwapima
viongozi wanaowajali.
Amesema Abwao amefika
wakati mzuri ambao wanawake wanahitaji kukombolewa na wimbi la umasikini ambalo
lilionekana kama halina dawa.
Hata hivyo amewataka akina mama wenzake kuwa waaminifu katika mikopo ili kuweza kusadia mikakati ya kujikwamua inasonga mbele.
CHANZO BLOG YA MATUKIO DAIMA
0 comments:
Post a Comment