Home » » PSPF YAWASAIDIA WANAFUNZI WANAOLALA SAKAFUNI

PSPF YAWASAIDIA WANAFUNZI WANAOLALA SAKAFUNI

KATIKA kukabiliana na changamoto za sekta ya elimu mfuko wa Pensheni kwa watumishi wa Umma -PSPF umekabidhi mabati 100 pamoja na mifuko ya saruji 150 vifaa vyenye thamani zaidi ya shilingi Milioni 2. 5 kwa shule ya sekondari Mlowa iliyopo katika halmashauri ya Wilaya ya Iringa.
Akikabidhi msaada huo meneja wa PSPF Msafiri Mugaka amesema hatua hiyo imekuja baada ya kutambua uwepo wa changamoto mbalimbali katika shule hiyo na wao kama jamii kuamua kuisaidia shule hiyo.
Aidha Mugaka amesema shule hiyo imekuwa na matatizo ya majengo na hivyo PSPS kama walezi na waandaaji wa watumishi wa kesho wameona ni vyema kushiriki kikamilifu katika kutatua tatizo hilo.
Akipokea msaada huo Kaimu mkuu wa Wilaya ya Iringa Gerlad Guninita amesema msada huo wa PSPF ni mkubwa kwani umewasaidia wanafunzi kuwaepusha na hali ya kukosa mabweni na hivyo kuwafanya kukosa muda wa kutosha wa kujisomea.
Shule ya sekondari Mlowa inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya wanafunzi kulala katika sakafu ya vyumba vya madarasa hali itokanayo na kukosekana kwa mabweni na vitanda.

0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Iringa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa