Home » » Waziri Mwakyembe atembelea Maeneo yaliyotumika harakati za Ukombozi na ya kihistoria Mkoani Iringa

Waziri Mwakyembe atembelea Maeneo yaliyotumika harakati za Ukombozi na ya kihistoria Mkoani Iringa

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akisalimiana na Chief wa kihehe Evaristo Sambiligunga Mwambeta alipokutana na machief wa kihehe kuzungumza nao kuhusu namna ya kuhifadhi historia ya ukomboziwa Bara la Afrika kwa vizazi vijavyo jana Mkoani Iringa
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) akizungumza na Machief wa kihehe (hawapo pichani) alipokutana nao kuzungumzia namna ya kuhifadhi historia ya ukombozi wa Bara la Afrika kwa vizazi vijavyo jana Mkoani Iringa
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (wapili kulia) katika picha ya pamoja na machief wa kihehe baada ya kuzungumza nao kuhusu namna ya kuhifadhi historia ya ukomboziwa Bara la Afrika kwa vizazi vijavyo jana Mkoani Iringa
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (watatu kushoto) akiwasili katika makumbusho ya Mtwa Mkwawa yaliyopo Kalenga kwa ajili ya kuona naoma makumbusho hiyo inavyohifadhi na kuendeleza historia ya shujaa Mkwawa aliyepigana vita vya msituni wakati wa harakati za kuwakomboa wahehe kutoka kwa utumwa wa wajerumani jana Mkoani Iringa. Watatu kulia ni Mratibu wa Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika Bibi. Ingiahedi Mduma
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (wapili kushoto) akiangalia fuvu la Mtwa Mkwawa alipotembelea makumbusho ya Mkwawa yaliyopo Kalenga kwa ajili ya kuona naoma makumbusho hiyo inavyohifadhi na kuendeleza historia ya shujaa Mkwawa aliyepigana vita vya msituni wakati wa harakati za kuwakomboa wahehe kutoka kwa utumwa wa wajerumani jana Mkoani Iringa.
Mtaalamu kutoka makumbusho Mkwawa (kulia) akimuonyesha Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Harrion Mwakyembe (wapili kulia) baadhi ya vifaa alivyotumia Mtwa Mkwawa wakati wa harakati za kuwakomboa wahehe kutoka katika utumwa wa wajerumani jana katika makumbusho ya Mkwawa iliyopo katika Halmashauri ya Iringa Mkoa wa Iringa.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akiwa ameshika silaha za jadi alizokuwa anatumia Mtwa Mkwawa wakati wa harakati za kuwakomboa wahehe kutoka katika utumwa wa wajerumani jana katika makumbusho ya Mkwawa iliyopo katika Halmashauri ya Iringa Mkoa wa Iringa.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akiangalia kaburi la Mtwa Abdul Adam Sapi Mkwawa alipotembelea makaburi ya machief kutoka ukoo wa Mkwawa jana katika makumbusho ya Mkwawa iliyopo katika Halmashauri ya Iringa Mkoa wa Iringa.
Mwanafunzi kutoka Shule ya Msingi Muungano akijibu swali la kihistoria lililoulizwa na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe wakati wa ziara yake katika mnara wa Frelimo ulipo katika shule ya Muungano jana Mkoani Iringa
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Msingi Muungano iliyopo katika mnara wa Frelimo alipotembelea mnara wa Frelimo uliojengea na serikali ya Tanzania mwaka 1977 kwa lengo la kutoa heshima na kumbukumbu kwa aliyekuwa kiongozi wa chama cha ukombozi nchini Mozambiki Bw. Samora Machel.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (watatu kushoto) katika picha ya pamoja na viongozi kutoka Halmashauri ya Iringa katika mnara wa Frelimo uliojengea na serikali ya Tanzania mwaka 1977 kwa lengo la kutoa heshima na kumbukumbu kwa aliyekuwa kiongozi wa chama cha ukombozi nchini Mozambiki Bw. Samora Machel.

Mhadhiri kutoka chuo kikuu cha Tumaini Dkt. Gibson Sanga (kushoto) akimuonyesha Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) baadhi ya vifaa vya kitamaduni vinavyotumiwa na kabila la wahehe alipotembelea makumbusho ya Iringa jana Mkoani Iringa.Picha na: Genofeva Matemu – WHUSM

0 comments:

 
Powered by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Iringa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa