Halmashauri ya mji wa Mafinga
imepitisha rasimu hiyo ya bajeti ya maendeleo katika kikao cha baraza la waheshimiwa madiwani kilichofanyika
26/2/2018 katika ukumbi wa halmashauli ambapo jumla ya fedha kiasi cha shilingi
bilioni 25.9 zilipitishwa.
Akiwasilisha rasimu hiyo ya bajeti kwa wajumbe wa
kikao hicho kwa niaba ya mkurugenzi Afisa
mipango wa halmashauri ndugu Andambike kyomo amesema halmashauri ya mji wa
mafinga imejipanga katika kuboresha namna ya utoaji wa huduma bora kwa wananchi
kwa kujikita katika vipaumbele vitano vya halmashauri ambavyo ni kuboresha
makusanyo mapato ya ndani ili kujenga stendi ya kisasa eneo la kinyanambo na
kuboresha mazingira ya uwekezaji na ujenzi wa viwanda,pili ni kuboreshakwa
kutenga fedha ili kugharamia uendeshaji ujenzi na ukarabati wa vituo vya
kutolea huduma za afya na elimu.
Afisa mipango ndugu Kyomo alindelea kuwasilisha kipaumbele cha tatu
kuwa ni kuboresha utendaji kazi wa watumishi wa umma kwa kutenga fedha kwa
ajili ya ununuzi wa vifaa vya kufanyia kazi,ujenzi wa nyumba za watumishi na
kutenga fedha za mishahara kwa kuzingatia ikama wakati kipaumbele cha nne ni
kuboresha uratibu, usimamizi na utekelezaji wa shughuli mbalimbali zinazotolewa na halmashauri kwa wananchi kwa
kutenga fedha za kutosha kwa ajili ya ununuzi wa magari matatu (3) ya
kuimarisha usimamizi na ufuatiaji huku kipaumbele cha tano ikiwa ni kuimarisha
utawala bora kwa kufanya vikao vya kisheria vya halmashauri na kuimarisha
mifumo ya utendaji.
Lengo kuu la bajeti ni kutekeleza
malengo ya dira ya Taifa ya maendeleleo 2025 na malengo ya milenia na mpango wa
maendeleo endelevu (SDG’s) ambapo kwa pamoja yanaelekeza kupunguza umasikini
iliokithiri na njaa,elimu ya msingi kwa wote,usawa wa kijinsia,kupunguza vifo
vya watoto, kupunguza vifovya uzazi, utunzaji wa mazingira,kukabiliana na janga
la UKIMWI na kujenga uchumi imara wenye kuhimili ushindani.
Mambo mengine muhimu yaliyozingatiwa
katika uandaaji wa bajeti ni pamoja na
Hotuba ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dk. John Pombe
Joseph Magufuli wakati akifungua rasmi Bunge jipya la Jamuhuri ya Muungano wa
Tanzania,Dodoma tarehe 20 Novemba 2015 ambayo pamoja na mambo mengine
inaelekeza kupunguza kero na kusogeza huduma kwa wananchi.
0 comments:
Post a Comment