Mwenyekiti
wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP) Abdul Nondo kwa mra ya kwanza
amefunguka na kuwashukuru watanzania baada ya kuachiwa kwa dhamana
katika mahakama ya Hakimu Mkazi, Mkoa wa Iringa leo Machi 26, 2018
Nondo
ameweka wazi hayo baada ya kuachiwa huru na kusema kuwa sasa anaweza
kuendelea na masomo yake pamoja na kesi hiyo ambayo itakuwa ikiendelea
mkoani Iringa.
"Namshukuru
sana wakili Jebra Kombole na wakili wangu mwingine wa Iringa mbali na
hapo napenda kuwashukuru wadhamini wangu kwa sababu masharti ya dhamana
yalikuwa yanahitaji wadhamini kutoka mkoa wa Iringa kwa hiyo nimepata
wadhamini mkoa wa Iringa Mungu awabariki sana.
"Saizi nipo huru naweza kwenda kuendelea na chuo huku nikiendelea na kesi mkoa wa Iringa.
"Pia
nawashukuru Afisa Magereza kwenye eneo ambalo nilikuwa nikiishi katika
kusubiria dhamana wamenitunza vizuri kwa upendo na ushirikiano mkubwa
hivyo nawashukuru wazazi wangu na Watanzania Mungu awabariki sina zaidi
ya zaidi ya hayo" alisema Nondo
Kesi
ya Abdul Nondo itatajwa tena tarehe 10 mwezi wa nne mwaka huu mkoani
Iringa ambapo wataanza kusikiliza hoja za awali, wakili wa Nondo
amewataka watanzani kuwa na subira juu ya jambo hilo kwa kuwa tayari
lipo mahakamani hivyo litafahamika.
0 comments:
Post a Comment