Mbunge
wa jimbo la Mufindi kaskazini Mahamuod Mgimwa aikiongea na baadhi ya
walimu wa shule za sekondari na shule za msingi jinsi gani ya kutatua
kero zilipo shuleni ili kuongeza ufaulu kwa wanafunzi
Mbunge
wa jimbo la Mufindi kaskazini Mahamuod Mgimwa akiwakabidhi zawadi ya
mbuzi kwa walimu wa shule za msingi waliofanya vizuri katika moja ya
kata iliyopo jimboni kwake.
Na Fredy Mgunda-Iringa
Wananchi
wa jimbo la Mufindi kaskazini wametakiwa kuwapeleka watoto wao shule
kwa lazima kwa kuwa elimu inatolewa bure na serikali ya awamu ya tano
chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Mafuli
kwa lengo la kuhakikisha kila mwanafunzi wote waweze kupata elimu na
kuondoa ujinga na kuleta maendeleo kwa taifa.
Hayo
yamesemwa na mbunge wa jimbo la Mufindi kaskazini Mahamuod Mgimwa
alipokuwa kwenye ziara ya kukagua miundombinu ya shule zilizopo katika
jimbo hilo ili kuweza kuzitatua changamoto zilizopo katika maendeo hayo.
Akiwa
bado yupo kwenye ziara hiyo mbunge huyo aligundua kuwa wazazi wengi
wamekuwa kikwanzo cha kuwapeleka shule watoto wa hivyo akawataka
viongozi wote wa serikali za vijiji kuwa chukulia hatua wazazi ambao
hawatawapekeka shule watoto wao.
Mgimwa
alisema kuwa yupo tayari kunyimwa kura na wananchi ambao atawachukulia
hatua za kisheria kwa kutowapeleka shule watoto wao kwa ajili ya faida
ya maisha yao.
“Nasema
kweli nitakubali kuachia ngazi ya kuwa mbunge kwa kunyimwa kura za
wananchi wasiopenda maendeleo ya watoto wao,hadi sasa shule zimefungua
lakini wazazi hawawapeleki shule watoto nitahakikisha wanachukuliwa
hatua za kisheria” alisema Mgimwa
Aidha
Mgimwa alisema kuwa sasa imefika mwisho kwa watoto wa jimbo la Mufindi
Kaskazini kuwa soko la wafanyakazi wa kazi za ndani wakati wanauwezo wa
kuwa viongozi hapo baadae.
“Nasema
tena haiwezekani kila mfanyakazi ukifika daresalaam utasikia katoka
Iringa jimbo la Mufindi Kaskazini sasa sitaki kusika swala hilo na
wazazi wanaofanya hivyo nitawachulia hatua za kisheria serikali ya awamu
ya tano inataka kuwa na wasomi wengi ili kuasaidia maendeleo ya
nchi”alisema Mgimwa
Mgimwa
alisema kuwa wazazi wa jimbo la Mufindi la Mufinda watafungwa kwa
kuwapeleka watoto wao kufanya kazi za ndani pindi wamalizapo shule ya
msingi au sekondari kufanya hivyo kunadumaza maendeleo yao.
“Haiwezekani
mwanafunzi amefaulu halafu mzazi anampeleka kufanya kazi za ndani
siwezi kukubali hata kidogo maana nimegundugua wazazi wengi hawapendi
watoto wao waendelee kusoma badala yake wanataka wakafanye kazi za ndani
narudia kusema mtoto akifaulu asipopelekwa shule nitamchulia hatua za
kisheria huyo mzazi” alisema Mgimwa
Mgimwa
aliwataka wanafunzi wakike kuacha kufanya ngono wakiwa na umri mdogo
ili kupunguza mimba za utotoni na kupoteza dira ya maisha wakiwa watoto
wadogo na kufanya hivyo kutawapelekea kufungwa jela kwa kuwa sheria
itachukua mkondo wake.
“Acheni
kufanya tendo la ndoa mkiwa na umri mdogo ili baadae mjenge maisha yetu
viongozi wengine wa wanawake wanavyofanya kazi serikalini na kwenye
mashirika mbalimbali ya nje ya nchi na ndani ya nchi”alisema Mgimwa
Mgimwa
aliwapongeza walimu wa shule za msingi za jimbo la Mufindi Kaskazini
kwa kuendelea kufanya vizuri kwenye mitihani ya kitaifa na kuendelea
kuitangaza vizuri jimbo hilo kupitia elimu.
“Kwa
kweli nisiwe mnafiki nichukue fursa hii kuwapongeza walimu kwa kufanya
vizuri maana kila mwaka elimu inazidi kukua katika jimbo la Mufindi
Kaskazi na kuendelea kuitangaza kitaifa” alisema Mgimwa
nao
baadhi ya walimu wakuu wa shule zilizopo jimbo la Mufindi Kazskazini
walisema kuwa wazazi wengi wamekuwa kikwazo cha maendeleo ya wanafunzi
kwa kuwakatisha tamaa juu ya umuhimu wa elimu.
“Hapa
katika kata hii ya Kibengu wazazi wengi hawapendi watoto wao kwenda
kusoma kwa kuwa watakuwa wanapunguza nguvu kazi zao mashambani ndio
maana hawawapatii mahitaji muhimu ya kuwasaidia wanafunzi kusoma kwa
uhuru” alisema walimu
Walimu
walimuomba mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini kutafuta wataalam wa
saikolojia kuja kuwapa elimu wazazi ili kukuza taaluma kwa wanafunzi wa
kata hiyo.“Ukiangalia
hali ya ufaulu wa shule hizi ni mzuri lakini kutokana na wazazi
kutokujua umuhimu wa elimu wamekuwa hawawapeleki watoto wao sekondari
wakifaulu mitihani ya shule ya msingi hivyo inapelekea upungufu wa
wanafunzi katika shule ya sekondari ya Ilogombe” alisema Walimu.
Mfikwa
alisema kuwa wamekuwa wakiitisha mikutano ya mara kwa mara lakini bado
tatizo kubwa hivyo jitihada zinahitajika kukomesha tabia hiyo kwa kuwa
bila hivyo watoto wa kata hiyo wataendelea kuwa wafanyakazi za ndani tu.
Zakayo
Kilyenyi ni diwani wa kata ya Kibengu alikiri kuwa wazazi wengi wa kata
hiyo hawana elimu juu ya umuhimu wa kujua dhamani ya elimu katika
maendeleo ya familia zao na taifa kwa ujumla.
“Kweli
kabisa wazazi wa kata ya Kibengu wamekuwa wakiwaambia watoto wasifanye
mitihani vizuri ili wasifaulu kwa kuwa wakifaulu watakuwa na gharama
kubwa ya kuwasomesha hivyo wakifeli wataenda kuwafanya kazi za ndani na
ndio furaha kwa wazazi wa kata ya Kibengu” alisema Kilyenyi
Kilyenyi
alisema kuwa uongozi wa kata ya Kibengu utaendelea kutoa elimu kwa
wazazi hao ili kurudisha morali ya kuendelea kuwapa mahitaji muhimu
yanayohitajika shuleni kwa kwa lengo la kuboresha maisha ya watoto hao.
“Zana
potofu zimekuwa kikwazo kikubwa sana katika maendeleo ya wananchi wa
kata ya Kibengu hivyo tukiondoa zana hiyo elimu itakuwa kwa wanafunzi wa
kijiji hichi” alisema Kilyenyi.
0 comments:
Post a Comment