Afisa
mipango wa Halmashauri isaya Mbenje, akimwonesha Mkandarasi Maeneo
mbalimbali ya kuyafanyia kazi katika chanzo cha Maji cha Sawala.
Mkurugenzi
Mtendaji Profesa Riziki Shemdoe na Mwenyekiti wa Halmashauri Festo
Mgina wakisaini Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Maji kwa gharama ya
shilingi Bilioni 1.8
Mkurugenzi
Mtendaji Profesa Riziki Shemdoe na Mwenyekiti wa Halmashauri Festo
Mgina, kushoto wakimkabidhi Mkataba Mkandarasi Siha Enterprises kulia
mara baada ya kusainiwa.
Na Afisa Habari Mufindi
Hatimaye
Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi imetiliana saini na Kampuni ya Siha
Enterprises Limited, kutekeleza ujenzi wa mradi mkubwa wa Maji Sawala,
wenye thamani ya shilingi bilioni 1.8, utakao wanufaisha wananchi wa
Vijiji vine vya Kata ya Mtwango baada ya kuikosa huduma ya Maji safi na
salama kwa miaka mingi.
Hafla
ya kihistoria ya kusaini kandarasi hiyo ya miezi 12, imefanyika katika
kijiji cha Sawala mbele ya viongozi wa Vijiji vinne vya Sawala, Mtwango,
Lufuna na kibao vinavyotarajiwa kunufaika na huduma hii muhimu kwa uhai
wa binadamu.
Akizungunza
mara baada ya kusainiwa kwa Mkataba huo, kaimu Mkuu wa Mkoa wa Iringa,
ambaye pia ndiye Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mh. Jamhuri William, amemtaka
Mkandarasi huyo kutekeleza mradi huo kwa ubora, kukamilisha kwa wakati
kadri ya mkataba aliosaini bila kuongeza gharama na ameahidi kuufuatilia
mradi huo kwa kila hatua ya ujenzi.
Mh.
Jamhuri pia, amewataka wananchi wa kata ya Mtwango kumpa shirikiano
Mkandarasi katika kipindi chote cha utekelezaji wa Mradi, huku akikemea
tabia ya uwizi kwa Vijana watakaopata ajira kwa kipindi chote cha
utekelezaji wa mradi huo uliosubiriwa kwa muda mrefu na wananchi wa kata
ya Mtwango.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Mh. Festo
Mgina, amesema Ofisi yake inaimani kubwa na Mkandarasi huyo na akamtaka
aanze kutekeleza ujenzi wa mradi kwa wakati kwani shauku pekee ya watu
wa Kata ya Mtwango, ni kupata huduma ya Maji baada ya Mkandarasi wa
awali kushindwa kukukidhi shauku yao.
Ujenzi
wa mradi wa Maji Sawala, utakelezwa na kampuni wa Siha Enterprises
Limited na utasimamiwa na Ofisi ya Maji Mjini Iringa (Iruwasa), Ofisi ya
Maji ya Katibu tawala Mkoa pamoja na Ofisi ya Maji ya Halmashauri ya
Wilaya ya Mufindi kwa muda usizidi miezi 12. Aidha, baadhi ya shughuli
kubwa zinazotarajiwa kutekelezwa ni pamoja na ujenzi wa Matenki manne ya
ujazo wa lita 450,000, kusambaza mabomba kwenye Vijiji husika pamoja na
kujenga vituo 122 vya kukinga Maji.
0 comments:
Post a Comment