Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Bw Exaud Kigahe mgombea ubunge jimbo la Mufindi kaskazini |
Exaud Kigahe |
Wanahabari wakimsikiliza Bw Kigahe wakati akitangaza nia ya kugombea ubunge |
MDAU mkubwa wa maendeleo ya elimu katika wilaya ya Mufindi mkoani Iringa na mzaliwa wa kijiji cha Nungwe, wilayani Mufindi Mkoani
Iringa Bw Exaud Kigahe ambae ni mchumi mkuu wa wizara ya viwanda na biashara amepania kuwakomboa kimaendeleo wakazi wa jimbo la Mufindi
Kaskazini linaloongozwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mahamudu
Mgimwa iwapo watamchagua kuwa mbunge wa jimbo hilo.
Akizungumza
na wanahabari juzi wakati akitangaza nia hiyo, Kigahe ambaye ni Mtaalamu wa
Takwimu anayefanya kazi katika Wizara ya Viwanda na Biashara jijini Dar es
Salaam alisema; “ni haki yangu kikatiba katika mchakato mzima wa demokrasia ya
kweli, nilifanya hivyo mwaka 2010 lakini kura hazikutosha nataka kuingia tena
mwaka huu.”
Katika
kura za maoni za CCM za mwaka 201, Mgimwa alipata kura 6,386 huku Mungai
akipata kura 3,430 na yeye (Kigahe) akiwa mshindi wa tatu kwa kupata kura
1,208.
Alisema
anataka kugombea ubunge katika jimbo hilo huku akifahamu kwamba wananchi wake
wengi ni masikini pamoja na wana
rasilimali za kutosha.
“Tuna
ardhi nzuri inayofaa kwa kilimo cha mazao mbalimabli ya chakula na biashara
kama chai, pareto na miti,” alisema.
Alisema
wakati wilaya hiyo ikiwa na shamba kubwa kuliko mengine yote ya miti nchini,
bado baadhi ya shule zake hazina madawati, milango na madirisha.
Alisema
anataka kuingia katika kinyang’anyiro hicho huku kipaumbele chake kikiwa ni
elimu kwani hazina hiyo ndio pekee inayoweza kusaidia kubadili maisha, uchumi
na maendeleo ya ujumla ya wilaya ya Mufindi.
“Watoto
wetu wakiwezeshwa, wakapata elimu bora wanaweza kushiriki kupambana na
umasikini kwa kutumia rasilimali zilizopo,” alisema.
Alisema
kwa muda mrefu jimbo la Mufindi Kaskazini limeendelea kupata viongozi wasio na
mbinu za kuibadili hali hiyo.
Aliyataja
maeneo mengine atakayoyapa kipaumbele endapo atashinda kura za maoni na
kuchaguliwa kuwa mbunge wa jimbo hilo kuwa ni pamoja na kuwashirikisha wananchi
na serikali kuboresha sekta ya afya, kilimo, maji, biashara, mawasiliano na
miundombinu ya barabara.
Na FGBLOG ,MUFINDI
Katika
Uchaguzi Mkuu wa 2010, Mgimwa aliwania ubunge wa jimbo hilo baada ya kumuangusha
katika kura za maoni, Joseph Mungai; kigogo aliyebahatika kushika uwaziri wa
wizara mbalimbali katika awamu za serikali zote ikiwemo ya serikali ya Mwalimu
Julius Nyerere na Jakaya Kikwete.
Katika
awamu ya kwanza ya Rais Jakaya Kikwete, Mungai alipata kuwa Waziri wa Kilimo,
Chakula na Ushirika kabla hajahamishiwa katika wizara ya Mambo ya Ndani.
0 comments:
Post a Comment