Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mkuu wa wilaya ya Mufindi Bi Mboni Mhita akifungua kongamano la Umoja wa wanawake Tanzania (UWT) wilaya ya Mufindi leo |
Washiriki wa kongamano la UWT wilaya ya Mufindi wakimshangilia mkuu wa wilaya ya Mufindi hayupo pichani |
Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Mufindi Bi Marcelina Mosha akimkaribisha mgeni rasmi |
Washiriki wa kongamano hilo wakifuatilia mafunzo ya afya na uzazi na yale ya ujasiliamali |
Katibu wa UWT Mufindi |
Viongozi wa UWT mkoa na wilaya pamoja na DC mufindi wakifuatilia mafunzo |
Mtaaluam wa afya akitoa semina ya afya kwa washiriki |
Mtaalam wa afya akitoa elimu ya matumizi sahihi ya kondom |
Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Iringa vijijini Bi Shakra kiwanga akitoa salam zake |
Na FgBlog Mufindi
MKUU
wa wilaya ya Mufindi mkoani Iringa Bi Mboni Mhita amewataka
wanawake kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi mbali mbali za uongozi
ikiwemo nafasi ya Urais katika uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi Octoba
mwaka huu
Alisema
ushindi wa wanawake katika nafasi mbali mbali ikiwemo ya udiwani
,ubunge na urais ni kubwa zaidi iwapo wanawake wenyewe watajiamini na
kuepuka na maneno ya
watu ambayo kimsingi wengi wao wanatamani kuona wanawake wakiwa nyuma
.
Bi
Mboni ambae ni mjumbe wa NEC Taifa alitoa rai hiyo leo katika ukumbi
wa CCM wilaya ya Mufindi wakati akifungua kongamano la umoja wa
wanawake Tanzania (UWT) alisema kuwa muda ukifika wanawake hawana
sababu
ya kuogopa kuingia katika nafasi mbali mbali za uongozi na kuwa
wale wenye uwezo wa kugombea udiwani ,ubunge na Urais wajitokeze
bila katika mapambano kuogopa .
Alisema
kikubwa si wanawake kuwatazama wenzao wanapoingia katika mapambano
ila ni kuona wanawake wanatengezeza jeshi moja la mapambano ya
kumsaidia kwa nguvu zote mwanamke mwenzao anayesimama katika kuwania
nafasi za uongozi.
Bi
Mboni alisema vijana pia hawana sababu ya kuchangamkia nafasi za
uongozi mbali mbali katika uchaguzi ujao badala ya kuwa nyuma na kuwa
kwa upande wake anajivunia kuwa mkuu wa wilaya ya Mufindi nafasi
ambae pia ni mkuu wa wilaya mwenye umuri mdogo zaidi kuliko wote
nafasi aliyeteuliwa na Rais Dr Jakaya Kikwete jambo ambalo anampongeza
Rais kwa uteuzi huo japo kabla ya uteuzi huo alikuwa ni makamu
mwenyekiti wa UVCCM Taifa .
Pia
alisema kuwa yeye pia ni miongoni mwa wajumbe wa NEC Taifa wadogo
zaidi ila pia alipata kuchaguliwa kuwa kiongozi wa vijana barani
Afrika na kuwa nafasi zote hizo amekuwa akizipata kutokana na
kuthubutu na kutojinyanyapaa kama mwanamke.
Hivyo
alisema wakati umefika wa vijana na wanawake nchini kutumia
nafasi ya uchaguzi mkuu wa mwaka huu kujitokeza kuwania nafasi
mbali mbali bila kuogopa .
Awali
akimkaribisha mkuu huyo wa wilaya kufungua kongamano hilo mwenyekiti
UWT wilaya ya Mufindi Bi Marcelina Mkini mbali ya kumpongeza mkuu
huyo wa wilaya ya Mufindi kwa utendaji wake mzuri bado alisema kuwa
wanawake katika wilaya ya Mufindi kwa mwaka huu wamejipanga
kugombea nafasi zote tatu ya udiwani ,ubunge na Urais
Kuwa
ushindi wa wanawake katika nafasi mbali mbali za uongozi utatokana
na ushirikiano mzuri wa wanawake wenyewe katika kuwaunga mkono
wale wote wanaogombea nafasi mbali mbali na kuwa falisafa ya UWT
Mufindi ni wanawake Kwanza .
Bi
Mkini ambae ni mjumbe wa NEC Taifa akiwakilisha wilaya hiyo ya
Mufindi alisema kuwa wanawake wa wilaya hiyo ya Mufindi
wamehamasishwa vya kutosha kuweza kujitokeza kugombea nafasi mbali
mbali za uongozi na kuwa mwitikio wa wanawake kuanza kuamka
kugombea nafasi za uongozi ulianza kuonekana katika uchaguzi wa
serikali za mitaa uliofanyika mapema hivi karibuni kwa wanawake
kuonyesha ushiriki mzuri katika mchakato huo.
Bila
kutaja kutaja idadi ya wanawake walioshinda katika uchaguzi huo
bado alisema matokeo mazuri ya uchaguzi wa serikali za mitaa ambayo
yaliiwezesha wilaya ya Mufindi kuongoza kwa mkoa wa Iringa kwa CCM
kushinda kwa zaidi ya aslimia 90 katika uchaguzi huo wa serikali za
mitaa ni moja kazi nzuri ya wanawake katika ushiriki wao katika
uchaguzi huo.
Kwani
alisema nguvu kubwa iliyoonyeshwa na wanawake wa wilaya hiyo ni
chachu ya kubadili mtazamo uliokuwepo wa wanawake kuendelea kuwa
madaraja ya kuvusha wanaume wanaogombea hivyo mtazamo huo kwa sasa
umeanza kupotea baada ya wanawake kuonyesha ushiriki wao katika
kugombea nafasi mbali mbali za uongozi .
Bi
Mkini alisema ushahidi wa nguvu ya wanawake katika kampeni upo
wazi katika wilaya hiyo ya Mufindi ambayo mkuu wa wilaya ni mwanamke
,mkurugenzi ni Mwanamke na mjumbe wa NEC Taifa ambae ni yeye mwenyewe
na kuwa nafasi hiyo aliipata baada ya kupambana na wanaume .
MWISHO
0 comments:
Post a Comment