Home » » MBUNGE AHOJI ZIARA ZA VIONGOZI NJE ZINA TIJA GANI KIUCHUMI.

MBUNGE AHOJI ZIARA ZA VIONGOZI NJE ZINA TIJA GANI KIUCHUMI.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa

Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa (Chadema) , amehoji ziara za viongozi nje ya nchi zinasaidia vipi kukuza uchumi wa nchi kulinganisha na gharama zinazotumika.
 
Akichangia bajeti ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kuhusu Makadirio, Mapato na Matumizi kwa mwaka wa fedha 2015/2016, jana bungeni, Msigwa alisema, tofauti na ziara za viongozi wa mataifa mengine ambao wanapokwenda nchi za nje wanatangaza uchumi na kutafuta masoko, Tanzania haifanyi hivyo.
 
“Alipokuja Rais Oboma hapa na ujumbe wake hakuja kushangaa shangaa, alikuwa na watu kutafuta sehemu za kuwekeza kwenye uchumi,” alisema.
 
Aidha, alisema balozi za Tanzania hazina utangazaji wa uchumi, na kutoa mfano wa ubalozi mmoja wa Tanzania nje ya nchi ambao umeiweka khanga kama kutangaza utalii badala ya kuweka mambo yanayoweza kutangaza fursa za biashara.
“Sisi utalii wetu ni kutangaza khanga na vitenge, hatuna utangazaji wa kiuchumi,” alisema.
 
Akizungumzia hali za balozi hizo nje ya nchi alisema zinasikitisha kutokana na kuwa hoi na zingine zinakosa hata magari, majengo yamechakaa na mengine yanatoa harufu. 
 
Akichangia wizara hiyo, Mbunge wa Ole (CUF), Rajab Mbarouk, alizungumzia ufisadi unaofanywa na wizara hiyo kwenye safari za viongozi na manunuzi ya tiketi.
 
Aidha, alisema baadhi ya watumishi waliomaliza muda wao kwenye balozi za Tanzania nje ya nchi wanaendelea kulipwa posho na mishahara.
 
Mbunge wa Chalinze (CCM), Ridhiwani Kikwete, alitaka wizara hiyo kuzungumia hali inayojitokeza kwenye mataifa mengine ya nje  ya unyanyasaji wa wageni.
 
Alisema Tanzania imekuwa ikishiriki katka ukombozi wa nchi za Afrika na kutoa mfano nchi ya Afrika Kusini, lakini chakushangaza Watanzania walioko huko wananyanyasika.
CHANZO: NIPASHE

0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Iringa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa