WATU wanne wasiofahamika wamewavamia wachimbaji wadogo wadogo wa madini aina ya dhahabu na kuwapora sh milioni nane.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Nyegesa Wankyo, alisema watu
hao walivamia machimbo hayo yaliopo Ihanzutwa, Tarafa ya Sadani, Wilaya
ya Mufindi, juzi majira ya saa 3 usiku wakiwa na gari aina ya GX 100
nyeusi ambayo haikutambulika namba zake.
Wankyo alisema watu hao walipofika walifyatua risasi hewani na kisha kuanza kupora fedha hizo na simu za mkononi.
Alisema Jeshi la Polisi mkoani hapa linaendelea kuwatafuta watuhumiwa hao na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria.
Katika tukio jingine, Hubiri Vaiga (32) ameuawa kwa kuchomwa na kisu sehemu ya ubavuni na Nisa Fodi (20).
Kamanda Wakyo alisema tukio hilo lilitokea juzi, saa 4 usiku katika
Kitongoji cha Mwingila, Kijiji cha Mbawi Masisiwe, Wilaya ya Kilolo.
Chanzo cha ugomvi ni ulevi, na mtuhumiwa anashikiliwa na polisi.

Chanzo;Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment