UTAFITI uliofanywa na Institute of Business Environment
Strengthening for Tanzania (IMED) kwa kushirikiana na Tanzania Chamber
of Commerce, Industries and Agriculture (TCCIA) Mkoa wa Iringa umebaini
Tanzania inapoteza mapato zaidi ya sh bilioni 174 kwa mwaka kutokana
na wakulima kutotumia mizani katika upimaji wa mazao ya mahindi na
mpunga.
Mwenyekiti wa chama cha wenye viwanda na wafanyabiashara, viwanda na
kilimo Tanzania mkoa wa Iringa TCCI , Lucas Mwakabungu, amebainisha
hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Maktaba
ya mkoa.
Mwakabungu alibainisha kuwa mikoa ya Iringa na Njombe pekee inapoteza
ushuru wa mazao (crop Cess) ya mahindi na mpunga zaidi ya shilingi
bilioni 2.5 kwa mwaka kutokana na mikoa hiyo kuhusika na kilimo cha
mazao hayo.
Alisema ushuru wa kodi ya mazao unaopotea kwa mazao ya mahindi na mpunga kwa nchi nzima kwa msimu ni shilingi bilioni 14.8.
Alisema utafiti uliofanywa na IMED ulichukua sampuli za magunia 43 ya
mpunga yaliyopimwa uzito na wakala wa vipimo na mizani (WMA) kati ya
magunia 482 yaliyokamatwa na kubainika kuwa uzito halisi wa kila gunia
ulikuwa wa wastani wa kilo 42 zaidi ya uzito unaostahili sawa na
asilimia 56.
Aidha alibainisha kuwa uzito wa wastani wa gunia la mahindi
lililojazwa kwa ndoo za plastiki lina kilo 36 zaidi ya uzito
unaostahili sawa na asilimia 40 kutokana na lumbesa ambayo wakulima
wanadidimizwa na wafanyabiashara.
Alisema wakulima wanatumia ndoo za plastiki na lumbesa kwa kuwa kuna
upungufu wa mizani na ushuru wa mazao kulipwa kwa gunia badala ya uzito
na kutokuwepo kwa vifungishio vinavyokubalika.
Mwakabungu alisema utafiti huo ilibainisha kuwa wakala wa vipimo na
mizani (WMA) hana rasilimali fedha za kutosha, vifaa vya kutosha na
hana rasilimali watu wa kutosha kuwezesha kuitekeleza sheria hiyo kama
inavyotakiwa.
Chanzo;Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment