Home »
» CHUO KIKUU CHA IRINGA CHAILETEA HESHIMA TANZANIA KATIKA SHINDANO LA TUZO YA HESHIMA YA SHERIA ZA VITA
CHUO KIKUU CHA IRINGA CHAILETEA HESHIMA TANZANIA KATIKA SHINDANO LA TUZO YA HESHIMA YA SHERIA ZA VITA
|
makamu Mkuu wa
chuo kikuu cha Tumaini Iringa, Prof Nicholaus Bangu kushoto akipokea
tuzo ya heshima ya sheria za vita kutoka kwa mkuu msaidizi wa kitivo
cha sheria Jane Massey huku wanafunzi walioshinda wakishuhudia
zoezi hilo leo |
|
Washindi wa tuzo
hiyo chuo kikuu cha Iringa wakiwa na tuzo yao kushoto ni mkuu wa chuo
Prof Nicholaus Bangu na kulia wa kwanza na mkuu msaidizi wa kitivo cha
sheria Bi Jane Massey |
|
mkuu msaidizi wa
kitivo cha sheria chuo kikuu cha Iringa Jane Massey akikabidhiwa tuzo
ya heshima ambayo chuo hicho kimeshinda katika mashindano
yaliyoshirikisha nchi saba Afrika na chuo hicho kunyakua tuzo hiyo
kwa kuwa chuo cha kwanza |
|
Mkuu wa chuo
cha Tumaini ( chuo kikuu cha Iringa ) Prof Nicholaus Bangu akionyesha
tuzo ya heshima ya sheria za kivita ambayo chuo chake kimeiwezesha
Tanzania kufanya vema |
|
Washindi wa tuzo hiyo wakiwa na vyeti vyao katika picha ya pamoja na mwalimu Dr Chachage
Tanzania yazibagwa nchi sita barani
Afrika katika mashindano ya vyuo vikuu ya kuwania tuzo ya heshima ya
sheria za vita yaliyomalizika hivi karibuni .
Katika shindano hilo lililofanyika
kati ya Novemba 16-23 mwaka huu jijini Arusha chuo kikuu cha
Iringa kiliwakilishwa na washiriki watatu ambao ni Anneny Nahum
,Janeth Nagai na Joanna Mcintype vijana hao waliweza kufanya vema
kiasi cha kuiwezesha nchi ya Tanzania kuibuka mshindi wa kwanza wa
tuzo hiyo.
Wakizungumza leo chuoni hapo katika
hafla fupi ya kukabidhi tuzo hiyo kwa uongozi wa chuo hicho
,washirikia hao walisema kuwa ushindi huo umetokana na ushirikiano
ulioonyeshwa na nidham iliyotukuka miongoni mwao.
Hata hivyo walisema kuwa tuzo hiyo ni heshima kubwa kwa Tanzania na ni heshima kwa chuo hicho .
mkuu msaidizi wa kitivo cha sheria
chuo kikuu cha Iringa Jane Massey alisema kuwa washiriki hao wamepata
kushinda kutokana na kuonyesha uwezo wa hali ya juu katika mashindano
hayo na kuwa heshima kubwa ambayo chuo hicho imepata ni jambo na
kujivunia na kumshukuru Mungu pia.
Alisema kinachoangaliwa katika
mashindano hayo na lengo la tuzo hiyo ni kuenzi amani na kuona hakuna
matukio ya ukiukwaji wa haki za binadamu ambayo yanatokea wakati wa vita
,hivyo sheria hiyo inapaswa kuendelea kutolewa hata kwa Tanzania
pia
Kwa upande wake makamu Mkuu wa chuo
kikuu cha Tumaini Iringa, Prof Nicholaus Bangu alisema kuwa chuo
hicho kitaendelea kufanya vema si katika mashindano pekee bali
katika mambo mbali mbali yakiwemo ya kitaalum .
Kwani alisema kuwa moja kati ya
mambo yanayozingatiwa katika ufundishaji chuoni hapo ni pamoja na
kuwafundisha wanafunzi katika maadili na nidham na ndio mafanikio ya
wanafunzi kufanya vema.
Tuzo hiyo ambayo inatolewa kama njia
ya kumuenzi aliyekuwa mwanzilishi wa msalaba mwekundi ilianzishwa
mwaka 2010 na kuanza kushindaniwa mwaka 2011 ambapo ilichukuliwa na
nchi ya Ephiopia ilinyakuwa kwa mara ya kwanza na mwaka 2012
ilichukuliwa na Kenya na mwaka huu Tanzania i meweza kuzishinda nchi
hizo sita ambazo ni South Afrika, Uganda,Kenya, Rwanda, Ethiopia na
Zimbabwe . Kwa Hisani ya Francis Godwin | k | | |
0 comments:
Post a Comment