Mdau
wa maendeleo katika jimbo la kalenga Iringa Bw Jackson Kiswaga
kushoto akikabidhi msaada wa madawati 30 yenye thamani ya zaidi ya Tsh
milioni 1 kwa mwenyekiti wa kijiji cha Lumuli Bw Mendrady Nywage kwa
ajili ya shule ya msingi Lumuli ,kulia ni diwani wa viti maalum tarafa
ya Kiponzero Vumilia Mwenda na wa pili kushoto ni diwani wa kata ya
Lumuli Charley Lutego pamoja na wajumbe wa serikali ya kijiji hicho
MDAU
wa maendeleo katika jimbo la Kalenga mkoa wa Iringa Jackson Kiswaga
ametoa msaada wa madawati 30 yenye thamani ya zaidi ya shilingi
milioni 1 katika shule ya msingi Lumuli ili kumaliza kero ya madawati
shuleni hapo.
Huku
akimpongeza Rais Jakaya Kikwete kwa kuendelea kuboresha sekta ya
elimu hapa nchini hata kufanikisha mpango wa shule za sekondari za
kata ambazo matunda yake yanaonekana kwa kila mmoja.
Akikabidhi
msaada huo leo Kiswaga ambae ni makazi wa jimbo hilo la Kalenga
alisema kuwa akiwa ni miongoni mwa wakazi wa jimbo la Kalenga
ameguswa na jitihada mbali mbali zinazofanywa na wananchi wa jimbo
hilo pamoja na mbunge wao Dr Wiliam Mgimwa .
Kwani
alisema kuwa mbali ya kazi nzuri inayofanywa na serikali ya chama
cha mapinduzi (CCM) chini ya mwenyekiti wake Taifa Rais Dr Jakaya
Kikwete bado watanzania wanapaswa kuendelea kutambua utendaji kazi
makini wa serikali ya CCM na pale wanapopata nafasi ya kuchangia
maendeleo ni vema kuunga mkono jitihada hizo.
"
Mimi kama mzaliwa wa kijiji cha Nyamihuu jimbo la Kalenga mbali ya
kuwa kwa sasa naishi jijini Dar es Salaam kwa kufanya shughuli zangu
za ajira ila bado natambua wazi kuwa bila CCM kuweka misingi
mizuri ya maendeleo katika elimu yawezekana leo nisingekuwa hapa nilipo
....hivyo kazi hii nayoifanya leo ni kuunga mkono kazi ya CCM"
Kiswaga
alisema kuwa akiwa kama mdau wa maendeleo ataendelea kusaidia jamii
ya mkoa wa Iringa kulingana na uwezo wake na kuwataka wakazi wengine
wa mkoa wa Iringa kukumbuka kurudi maeneo yao waliyozaliwa na
kusaidia shughuli za kimaendeleo zinazoibuliwa na wananchi.
Awali
mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Lumuli Bw Mendrady Nywage
alisema kuwa kijiji hicho kilimwomba Kiswaga kusaidia msaada huo
wa madawati pindi alipoalikwa kama mgeni rasmi katika mahafali ya
darasa la saba shuleni hapo.
Hata
hivyo alisema mahitaji halisi ya madawati ni 40 na kuwa tayari
Kiswaga ameahidi kusaidia madawati 10 yaliyosalia shuleni hapo na
hivyo kumaliza kabisa tatizo la madawati katika shule hiyo ya msingi
Lumuli.
Diwani
wa kata ya Lumuli Charlesy Lutego mbali ya kumpongeza Kiswaga kwa
msaada huo bado alisema katika kata yake kuna changamoto nyingi
ikiwemo ya majengo ya shule mbali mbali ya shule kukamilika kujengwa
bila kupauliwa kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa kutokana na kukosa
uwezo wa kununua mbao na bati zaidi ya 400 za kuezekea.
Na
francis godwin blog
0 comments:
Post a Comment