Ikiwa
leo ndio mapokezi rasmi ya Mwenge wa Uhuru kitaifa manispaa ya Iringa
,viongozi mbalimbali wamejitokeza kuupokea mwenge huo huku kesho
ikiwa ndo kilele cha Maadhimisho ya mwenge huku mgeni rasmi akiwa ni
rais wa Tanzania DK.JAKAYA MRISHO KIKWETE
Mwenge huo wa uhuru umepokelewa leo na
mkuu wa wilaya ya kilolo GERALD GUNINITA na
kumkabidhi mkuu wa wilaya ya iringa mjini RETISIA WARIOBA na
kuendelea kuzindua miradi mbalimbali ikiwemo kituo cha
michezo kwa vijana chini ya shirika la IDYDC ili kuendeleza michezo kwa vijana.
Akisoma hutuba kwa mgeni rasmi meneja wa kituo hicho cha
michezo LIGE MASANJA amesema kuwa lengo la kuanzisha kituo hicho cha
vijana ni kuona vijana wanapata maendeleo kupitia michezo na elimu
0 comments:
Post a Comment