Mwanafunzi
wa shule ya sekondari Idodi wilayani Iringa amelazwa katika Hospitali
ya Rufaa ya mkoa wa Iringa kwa madai ya kupigwa viboko zaidi ya 100 na
mtu anayedaiwa kuwa ni mwalimu wa shule hiyo na kufungiwa katika bweni kwa siku 3 ili kuificha siri hiyo.
Tukio
hilo linakuja wakati harakati mbalimbali za kijamii na asasi za kiraia
zikipiga kelele kupinga vitendo vya ukatili wakati jeshi la Polisi
likianzisha dawati la jinsia kwa ajili ya kutokomeza masuala hayo.
Ni
mwanafunzi Lusinde Nyaulingo, wa kidato cha tatu katika shule ya
sekondari Idodi, ambaye anaugulia maumivu makali katika Hospitali hii ya
rufaa ya mkoa wa Iringa, word namba tano ya majeruhi, kutokana na
ukatili uliosababisha majeraha sehemu mbalimbali za mwili wake, hasa
maeneo ya mapaja, makalio na mgongo, baada ya kupigwa kwa tuhuma za
kuchukua simu ya mwanafunzo mwenzie, jambo linalomfanya mwanafunzi huyu
apoteze muda mwingi wa masomo wakati akipatiwa matibabu ili kurudisha
afya yake.
Lusinde
anasema baada ya kuangushiwa kipigo hicho kikali, kilichodumu kwa zaidi
ya masaa tatatu, alipoteza fahamu na kisha kufungiwa katika bweni kwa
siku tatu, huku wanafunzi wenzie wakipigwa marufuku kufikisha taarifa ya
ugonjwa kwa wazazi wa Lusinde.
Hata
hivyo jeshi la polisi kupitia kamanda wake mkoa wa Iringa ACP Athmani
Mungi limesema kuwa wanafuatilia tukio hilo ili kuhakikisha haki
inatendeka, kwa kumchukulia hatua za kisheria mtuhumiwa ikiwa ni pamoja
na kumfikisha Mahakamani.
http://bongoleotz.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment