Home » » HAMDUNI - ACHENI FIKRA POTOFU JUU YA ELIMU YA WATU WAZIMA

HAMDUNI - ACHENI FIKRA POTOFU JUU YA ELIMU YA WATU WAZIMA

 Bango la maadhimisho ya siku ya Elimu ya watu wazima, katika kijiji cha Ikuvilo, Kata ya Luhota Wilaya ya Iringa. 
 Ofisa elimu ya Watu wazima Wilaya ya Iringa Bi. Asha Hamduni akitoa taarifa ya utekelezaji wa elimu ya watu wazima katika kijiji cha Ikuvilo Wilaya ya Iringa.
 Mgeni rasmi wa sherehe ya elimu ya watu wazima, makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Mh. Costantino Kihwele akikagua mabanda ya wadau wa elimu ya watu wazima katika maadhimisho ya siku ya hiyo.
 Bw. Joachim Mgimwa (wa pili kulia) mmoja wa wageni waalikwa wa hafla ya siku ya elimu ya watu wazima iliyofanyika katika Kijiji cha Ikuvilo Wilaya ya Iringa.
 Baadhi ya wadau wa elimu ya watu wazima wakiwa katika sherehe hiyo.
Makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Mh. Costantino Kihwele akiwahutubia wananchi waliofika katika siku ya elimu ya watu wazima. Johachim Mgimwa akitoa ujumbe kwa wanavikundi wa Vicoba sita wa Kata ya Luhota waliokuwa nao wakizindua vikundi hivyo katika maadhimisho hayo ya siku ya elimu ya watu wazima. Johachim alifika katika hafla hiyo akimwakirisha Waziri wa fedha Dr. Willium Mgimwa ambaye ni mbunge wa jimbo hilo la Kalenga, ambapo vikundi hivyo vilichangiwa jumla ya shilingi Milioni 8 ya ahadi.
 Wanafunzi wa chuo cha ufundi cha Ukombozi kilichopo Nyabula katika Wilaya ya Iringa, wakiunga mkono harakati zinazofanywa na elimu ya watu wazima, (mwenye shati la Draft ni mkurugenzi wa chuo Bw. Deo Chengelela.
 Makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Mh. Costantino Kihwele akiwa na jopo la viongozi wa Halmashauri hiyo wakikagua mabanda ya maonyesho katika siku ya elimu ya watu wazima.  
Mkurugenzi wa chuo cha ufundi Ukombozi Bw. Deo Chengelela akitoa taarifa ya chuo chake kwa Mh. Kihwele katika maadhimisho hayo ya siku ya elimu ya watu wazima.       
 Mh. Kihwele akitoa maagizo kwa viongozi wa Halmashauri kuhakikisha wadau hao wanaungwa mkono na serikali katika kuongeza ajira kwa vijana kwa kutoa elimu ya ufundi kwa jamii. 

Baadhi ya wanafunzi, mwalimu na mkurugenzi wa chuo cha Ufundi Ukombozi wakiwa katika banda lao wakionyesha baadhi tu ya bidhaa wanazotengeneza katika idara ya ufundi wa kushona.
 Mh. Kihwele akizungumza na kikundi cha akiba na mikopo cha Vicoba moja ya vikundi sita vilivyozinduliwa katika siku hiyo ya elimu ya watu wazima.

 Bw. Bonus Fivawo mkazi wa Nyabula, aliyefika katika kijiji cha Ikuvilo kuunga mkono maadhimisho ya siku ya elimu ya watu wazima.
 Bw. Bonus Fivawo akionyesha moja ya mazao (Aloveira).
 Bw. Bonus Fivawo akionyesha zao la Zukini (Zuchini) ambalo pia hutumiwa kama dawa.
 Mmea aina ya Boga (Zuchin) unaoliwa tunda na majani yake huku ukiwa ni sehemu ya tiba.
 Mkaguzi mkuu wa shule Bi. Martha Silavwe na viongozi wengine wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, wakishangilia jambo katika siku hiyo ya elimu ya watu wazima.
 Bi. Martha Silavwe akitoa ujumbe katika hafla hiyo.
 Bi. Asha Hamduni ofisa elimu ya watu wazima (Katikati) akifuatilia jambo katika sherehe hiyo ya elimu ya watu wazima.
 Mzee wa Kihehe akiwaunga mkono kikundi cha watoto 9 wa familia moja, kinachojihusisha na Utamaduni wa ngoma ya Kihehe "Njuga au Mangala).
 Mmoja wa wazee wa kabila la Wahehe  akifurahishwa na ngoma ya watoto, ya kabila lake "Hehe" baada ya watoto hao kutia fora katika maadhimisho hayo na kumfanya kila moja kuvutiwa nao.
   Kweli Mtoto wa Nyoka ni Nyoka,  Watoto hawa wakisakata haswa ngoma ya Njuga, ambapo kila mmoja aliyeguswa  aliamua kutoficha hisia zake kwa kuinuka na kucheza.
 Naye Bw. Johachim Mgimwa hakuvumilia uhondo wa "Livangala" au Njuga
 Bw. Johachim Mgimwa naye anaamua kulisakata Livangala, chezea Njuga wewe!!??.
   Bila ajizi watu walimwaga fedha kwa kundi hilo la watoto, kwa kuunga mkono jitihada zao za kudumisha Mila ya Wahehe.
 Mratibu wa VICOBA Mkoa wa Iringa Bi. Tisiana Kikoti akisoma taarifa ya Vicoba sita vya Kata ya Luhota, vikundi vyenye lengo la kuanzisha Benki ya Kata Luhota, aliyeshika Mic (Kisemeo) ni afisa Utamaduni wa Wilaya ya Iringa.
 Viongozi wa Vikundi sita vya Vicoba Kata ya Luhota wakiwa katika Picha ya pamoja mara baada ya vikundi vyao kuzinduliwa rasmi na Johakimu Mgimwa aliyemwakirisha Waziri Mgimwa ambaye ni mbunge wa jimbo hilo la Kalenga, (mwenye suti) ni Mratibu wa Vicoba mkoa wa Iringa Bi. Tisiana Kikoti.

 <<<<<<<<<<<<HABARI>>>>>>>.
JAMII imetakiwa kuacha fikra potofu juu ya elimu ya watu wazima, kwa kuiona elimu hiyo ni maalumu tu kwa watu wasio jua kusoma, kuandika na kuhesabu (KKK).

Rai hiyo imetolewa na afisa elimu ya watu wazima Wilaya ya Iringa Bi. Asha Hamduni katika maadhimisho ya siku ya elimu ya watu wazima iliyofanyika katika kijiji cha Ikuvilo katika Kata ya Luhota Wilaya ya Iringa.

Bi. Hamduni amesema ipo haja kwa jamii kubadili fikra hiyo, kwani elimu hiyo sasa inaendana na wakati na kuwa inatolewa pia kwa wanafunzi waliohitimu elimu ya darasa la saba na kushindwa kendelea na masomo ya elimu ya sekondari.

Aidha Bi. Hamduni amesema awali elimu hiyo haikuwa na tija kwa baadhi ya walengwa kutokana uwepo wa vitabu vinavyofundisha masomo ambayo hayawafai baadhi ya wananchi wa Mikoa mingine.

Akitolea mfano wa kitabu kilichokuwa kinafundisha kilimo cha zao la Korosho Mtwara, Bi. Hamduni amesema vitabu hivyo havikuwa na tija kwa wananchi wa mikoa ambayo haijihusishi na kilimo hicho na hivyo kisomo cha elimu ya watu wazima kupuuzwa.

Pia amesema baadhi ya changamoto zinazoikabiri idara ya elimu ya watu wazima ni pamoja na utoro kwa watu maarufu ambao huona aibu kuhudhuria masomo hayo, huku  malipo duni (Honoralia) ya shilingi elfu 20 kwa mwezi nayo yakichangia kuwakatisha tamaa walimu wanaotoa elimu hiyo.

Hata hivyo amesema Wizara kupitia idara ya elimu watu wazima imebadili mfumo wa masomo huku masomo ya masafa marefu pamoja na elimu ya ufundi stadi ukiwahusisha watu wa elimu mbalimbali.

0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Iringa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa