BAADHI ya wanafunzi wa darasa la saba wakiwemo
watoto yatima wa Shule ya Msingi Kimala, kata ya Kimala wilaya ya Kilolo,
mkoani Iringa, huenda wasifanye mitihani yao mwisho kutokana na kukosa michango
ya sh 47,000 ambayo wanadaiwa shuleni hapo.
Baadhi ya wanafunzi hao wameliambia gazeti hili
kuwa uwezekano wa kutokufanya mitihani upo kutokana kwani hivi sasa
hawaruhusiwi kuingia madarasani na madala yake hufanyishwa kazi za nje.
Wanafunzi waliozungumza kwa sharti la kutotaja
majina yao, walisema kuwa wamekuwa wakifanyishwa kazi na uongozi wa shule
badala ya kusoma kwa sababu hawajalipa michango.
Walifafanua kuwa walizuiliwa kufanya mitihani ya
kanda jambo ambalo wananchi walilipigia kelele na kulazimishwa kufanyishwa
mitihani saba kwa siku mbili.
Wakizungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti,
wananchi wa kijiji hicho walisema mwalimu mkuu wa shule hiyo amekuwa mbabe
kutaka kila anachokitaka kifanyike pasipo makubaliano na wazazi au kamati ya
shule.
Boniface Kasuga ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya
shule hiyo alieleza kushangazwa na michango hiyo kuwa ni mipango ya watu
binafsi.
“Hii michango ni ya uonezi. Mchango wa darasa la
saba unakujaje kwa kila mwanafunzi kutozwa sh 47,000?
“Kuna watu wachache ambao wanapanga michango hiyo
kama ulaji kwao,” alisema Kasuga.
Mweyekiti wa kamati ya shule hiyo Telaki Ndenga
amethibitisha kuwepo kwa michango hiyo na kwamba kamati ya shule haijawahi
kushirikishwa juu ya michango hiyo.
Mitihani ya darasa la saba inatarajiwa kuanza
Septemba 12, mwaka huu.
Chanzo: Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment