Home » » MKUU WA MKOA WA IRNGA DR.CHRISTINE ISHENGOMA ASISITIZA UMUHIMU WA UTOAJI WA HUDUMA YA CHAKULA CHA MCHANA MASHULENI

MKUU WA MKOA WA IRNGA DR.CHRISTINE ISHENGOMA ASISITIZA UMUHIMU WA UTOAJI WA HUDUMA YA CHAKULA CHA MCHANA MASHULENI

mkuu wa mkoa wa iringa Dr.Christine Ishengoma
Mkuu wa mkoa wa iringa dr.Christine Ishengoma ameyasema hayo leo ofisini kwake alipokutana na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali mkoani iringa,Aidha amewataka wananchi wa mkoa wa iringa kujitoa kikamilifu ili kufanikisha huduma hiyo mashuleni amesisitiza kuwa chakula kitakapo patikana mashuleni kiwango cha elimu kitakuwa kutokana na kuwepo kwa usikivu wakati wa somo na ufaulu mzuri wa wanafunzi,pia amezitaka kamati za shule kukaa na wazazi na kuwaelimisha juu ya umuhimu wa chakula cha mchana mashuleni na kutafuta njia nzuri ya uchangiaji.
 Aidha ametoa takwimu za shule ambazo zinatoa chakula cha mchana mashuleni,ambapo mkoa wa Irnga una jumla ya ya shule za msingi 481 na 151 za sekondari,kwa upande wa wa shule za msingi iringa manispaa zipo shule 49,zinazotoa chakula ni 21,iringa vijijini zipo shule 145,zinazotoa chakula ni 129,kilolo zipo shule111 zinazotoa chakula ni 98,mufindi zipo shule 176 zinzotoa chakula ni 72,na hivyo kufanya jumla ya shule 320 zinzotoa chakula kati ya shule 151 zilizopo.NAkwa upande wa shule za sekondari,iringa manispaa sipo shule 26 zinzotoa chakula ni 11,iringa vijijini zipo shule 32,zinazotoa chakula ni 21,kilolo zipo shule 38 zinazotoa chakula ni 19,mufindi zipo shule 55 zinazotoa chakula ni 36,na hivyo kufanya jumla ya shule87 zinazotoa chakula kati ya shule 151 zilizopo
 
CHANZO: FRANCIS GODWIN MZEE WA MATUKIO DAIMA BLOG

0 comments:

 
Powered by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Iringa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa