Aliyekuwa naibu meya wa manispaa ya Iringa G. Ndaki akiomba kura kwa wajumbe kabla ya kujiuzulu
Katibu wa Chadema wilaya ya Iringa mjini Suzana Mgonakulima na diwani
wa kata ya Mvijeni Frank Nyalusi wakifuatilia zoezi zima la uchaguzi
,Mgonakulima ni diwani wa viti maalum pia
Leo
umefanyika uchaguzi wa Naibu Meya katika manispaa ya Iringa, ambapo ushindi katika uchaguzi huu amekuwa ni
GEREVAS NDAKI ambaye alikuwa akishikilia nafasi hiyo toka awali.
Uchaguzi huo
umefanyika katika kikao cha baraza la madiwani wa manispaa ya iringa ambapo umeambatana na kamati mbalimbali za
baraza hilo ikiwemo kamati ya afya, mazingira fedha na nidhamu.
Katika uchaguzi
huo ni mugombea mmoja tu ambaye aliwania nafasi hiyo kupitia chama cha
mapinduzi ccm na wajume 23 ndio walishiriki katika uchaguzi huo na kura moja
iliharibika.
Kwa upande
wake naibu meya aliyechaguliwa amewashukuru wote waliomchagua na kusema kwa
hata hiyo kura moja ambayo haijamchagua anaishukuru pia kwani inatokana na na
mhusika kutoridhika na kazi ya ke hivyo bado anaowajibu wa kujipanga upya ili
aweze kumfanya mtu huyo akubaliana na uwajibikaji wake.
KWA HISANI YA FRANCIS GODWIN NA JIACHIE BLOG
0 comments:
Post a Comment