Home » » MKUU WA MKOA WA IRINGA AONGOZA MAMIA YA WAKAZI WA IRINGA KATIKA MAZISHI YA MMOJA KATI YA WANAJESHI 7 WALIOUWAWA DARFUR

MKUU WA MKOA WA IRINGA AONGOZA MAMIA YA WAKAZI WA IRINGA KATIKA MAZISHI YA MMOJA KATI YA WANAJESHI 7 WALIOUWAWA DARFUR

 Mkuu  wa  mkoa  wa  Iringa Dr  Christine Ishengoma  akitoa  heshima ya mwisho  katika mwili wa marehemu Koplo Owald Chaula  leo
 Wanajeshi  wakiuandaa mwili  wa mwenzao
Wananchi   na ndugu  wa Chaula  wakilia kwa uchungu
 Wananchi  wakitoa  heshima  zao  za mwisho

 Mkuu  wa  wilaya ya  Kilolo Gerald Guninita  kutoka kushoto ,mkuu  wa mkoa  wa Iringa Dr Ishengoma na mwenyekiti  wa CCM  wilaya ya  Kilolo Sety Mwamoto  pamoja na kamanda wa  polisi mkoa  wa Iringa Ramadhan Mungi  wakiwa katika  msiba  huo
 DC  Kilolo Bw  Guninita  akitoa heshima  zake  akifuatiwa na mwenyekiti wa CCM Kilolo SEty Mwamoto

 Mwili  wa askari  Chaula  ukielekea  makaburini 
 Mwili  huo  ukishushwa  kaburini
 Heshima  za  mwisho  za kijeshi  kwa marehemu Koplo Oswald Chaula
 Mkuu wa mkoa  wa Iringa Dr  Ishengoma  akiweka  shada la maua 
 DC  Kilolo akiweka  shada la maua katika kaburi  hilo la marehemu Chaula  leo
 Mwakilishi  wa JWTZ  akiweka  shada la maua 
 Mkuu  wa  wilaya  ya  Kilolo  Bw Guninita  akiwafariji  wafiwa

 Mwenyekiti  wa CCM  Kilolo Bw Sety  Mwamoto wa tatu  kulia akiwa na  viongozi  wenzake  katika mazishi hayo picha na  Said Ng'amilo na  Francis Godwin wa matukiodaima.com
.................................................................................................................................................
MKUU  wa mkoa  wa  Iringa  Dr Christine  Ishengoma  leo aongoza mamia ya  wakazi  wa  wilaya ya  Kilolo mkoani Iringa  katika  mazishi  ya  askari  mmoja kati ya  askari  7  wa jeshi la  wananchi Tanzania (JWTZ) waliouwawa katika shambulio la ghafla   Darfur nchini Sudani marehemu  Coplo Oswald Chaule .

Mkuu  huyo  wa  mkoa  akiwa  ameongozana na  viongozi  mbali mbali  wa  chama na  serikali katika  wilaya ya  Kilolo na mkoa  wa Iringa ameongoza mazishi  hayo  katika  kijiji  cha Mtitu  wilaya ya  Kilolo  ,huku akitoa  ubani  wa Tsh 200,000 wakati  mkuu wa  wilaya ya  Kilolo  Gerald Guninita  akiwasilisha rambi rambi ya  wananchi  na  watumishi  wa  Kilolo  la Tsh 300,000 kwa  familia ya  askari  huyo.

Akitoa salam  za rambi rambi mkuu  huyo wa mkoa  alisema  kuwa  mkoa  wa Iringa na Taifa  limepoeza askari  shupavu ambao  wataendelea  kukumbukwa  kutona na mchango  wao katika  Taifa .

“ Mkoa wa  Iringa  umeondokewa na  kijana  shupavu  na mzalendo katika  Taifa  lake ambae  alijitoa  kwa  ajili ya kulitumikia  Taifa  ….hivyo  sisi kama serikali ya  mkoa  tutaendelea  kumuenzi marehemu kwa  uzalendo wake katika  taifa”

Mazishi  ya  wanajeshi  hao  yanafanyika  huku  ikiwa  imebaki  siku  moja  kwa  Taifa  kuadhimisha  siku ya mashujaa nchi ambapo katika  mkoa  wa Iringa  maadhimisho  hayo  hufanyika katika  viwanja   vya  bustani ya  manispaa ya  Iringa .

Wakizungumzia  juu ya  kifo  cha mwanajeshi  huyo  baadhi ya  viogozi  wa  vyama  vya  siasa na  serikali akiwemo  mwenyekiti  wa CCM wilaya ya Kilolo Sety Mwamoto  alisema kwa   vifo  vya  wanajeshi  hao  vimelitikisa  Taifa na kuwa  mchango  wao katika  Taifa  utakumbukwa  daima.
PICHA ZOTE NA FRANCIS GODWIN

0 comments:

 
Powered by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Iringa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa