Leo
ni siku ya maadhimisho ya mashujaa nchini Tanzania na kitaifa yamefanyika
katika mkoa wa kagera,ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Mh. RAIS WA JAMUHURI YA
MUUNGANO WA TANZANIA, JAKAYA KIKWETE.
Katika
mkoa wa Iringa maadhimisho hayo yamefanyika katika viwanja vya bustani ya
manispaa ya iringa na mgeni rasmi katika maadhimisho hayo alikuwa mkuu wa wilaya
ya kilolo GERALD GUNINITA badala ya mkuu wa mkoa wa Iringa CHRISTINE ISHENGOMA.
Akizungumza
katika maadhimisho hayo mkuu wa wilaya huyo amesema kuwa wanaadhimisha siku hii
ya leo kwa sababu ya kuwakumbuka mashujaa ambao walipigana uhuru wa taifa letu.
Guninita
amesema pia dhumuni la kuwa kumbuka mashujaa hao ni kwa sababu walikuwa
wakipambana dhidi ya Nduli Idiamini, ambaye alichokoza Taifa letu mwaka 1978.
Aidha
ameongeza kwa kusema kuwa wakazi wa iringa na watanzania kwa ujumla wanapaswa
kukumbuka kuwa mashujaa hao walikufa wakati wakipigania amani na uhuru wa taifa
letu hivyo ni muhimu kuwaenzi ili kudumisha amani yetu kwa faida ya kizazi cha
sasa na cha baadaye.
CHANZO: JIACHIE BLOG
0 comments:
Post a Comment