Home » » WASANII IRINGA WATOA USHAURI WA BURE KWA LULU WATAKA AOKOKE

WASANII IRINGA WATOA USHAURI WA BURE KWA LULU WATAKA AOKOKE

Wapenzi  wa  muziki  filam mkoani Iringa  wametoa onyo kwa msanii Elizabeth Michael maarufu Lulu aliyetoka kwa  dhamana  mahabusu kufuati  tuhuma ya kesi yake ya mauwaji ya msanii mwezake Stivin Kanumba ,kuwa anapaswa  kutumia muda huu kuwa  jirani ni kanisa badala ya  kupenda starehe za dunia.




Wakizungumza na mtandao huu  wa  www.francisgodwin.blogspot.com wasanii hao Johari John na Kevin Sanga  walisema  kuwa dhamana ya Lulu ni mapenzi ya Mungu  hivyo mbali ya  kutoka mahabusu kwa dhamana bado anapaswa  kuishi kwa utulivu zaidi muda  wote ikibidi kuanza  kuwa karibu na kanisa.

Hata  hivyo John alitaka  waumini wa madhehebu mbali mbali kuendelea  kumwombea msanii  huyo ili Mungu aendelee  kusimama upande  wake.

Wasanii hao  walisema  kuwa  suala la msanii  huyo  kuendekeza  kujirusha kwa  sasa asilipe nafasi katika maisha yake na badala yake  kumgeukia Mungu  zaidi na kuachana na mambo ambayo hayampendezi mwenyezi Mungu.

0 comments:

 
Powered by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Iringa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa