Home » » MTUHUMIWA WA MAUWAJI YA MWANGOSI KUFIKISHWA TENA MAHAKAMANI KESHO

MTUHUMIWA WA MAUWAJI YA MWANGOSI KUFIKISHWA TENA MAHAKAMANI KESHO



Huyu ndie mtuhumiwa wa mauwaji ya Daudi Mwangosi
MTUHUMIWA  wa  mauwaji ya aliyekuwa mwandishi wa habari wa kituo cha Chanel Ten mkoani Iringa marehemu Daudi Mwangosi askari  wa FFU mwenye namba G2573 Pasificus Cleophace Simoni (23)ambae  alishindwa kufikishwa mahakamani katika kesi yake  baada ya kudaiwa kuwa ni mgonjwa sasa atafikishwa  tena mahakamani kesho Januari 31.
Kesi   hiyo ambayo ilitajwa Januari 27 ambapo mtuhumiwa huyo hakuweza kufikishwa  mahakamani  hapo baada ya mahakama  hiyo  kuelezwa  kuwa mtuhumiwa   huyo ni mgonjwa na  imeshindikana  kufikishwa mahakamani hapo.
 
Mwendesha mashtaka  wa jamhuri Adolf Maganda aliieleza hakimu  wa mahakamani ya hakimu mkazi  wilaya ya Iringa Dyness Lyimo kuwa mtuhumiwa alipaswa  kufikishwa mahakamani hapo  Januari 27  ila ilishindikana  kutoka na taarifa  kuwa ni mgonjwa  hivyo  kuomba  kupangwa  tarehe nyingine ya kutajwa  kesi hiyo ambayo  bado  upelelezi wake  kukamilika .
Hata  hivyo mahakamani  hiyo  liahirisha  kesi hiyo  hadi  kesho Januari 31  itakapotajwa  tena .
Mtuhumiwa  huyo anatuhumiwa  kumuua kwa makusudi kwa   bomu aliyekuwa  mwandishi  wa habari wa Chanel Tena  mkoa  wa Iringa  marehemu Mwangosi  septemba 2 Septemba mwaka jana  katika kijiji cha Nyololo Wilaya ya Mufindi Mkoa wa Iringa  wakati  wa vurugu kati ya  polisi na wafuasi wa  Chadema .kinyume na kifungu cha sheria namba 148 kifungu kidogo 5A.i cha makosa ya jinai. Kwa mujibu wa kesi za jinai, sheria kifungu 196 kanuni ya adhabu Cap. 16 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2002,

0 comments:

 
Powered by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Iringa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa