| Kijana aliyekuwa akichunga mifugo hiyo akiwa hana shaka |
Magari yakipita kwa shida eneo hilo kuhofu ng'ombe hapo kuvuka barabara
Pamoja na Halmashauri ya manispaa ya Iringa mkoani Iringa kuweka sheria ya kuzuia mifugo kuzagaa katikati ya mji wananchi wameendelea kupuuza sheria hiyo kusudi na kugeuza maeneo ya kandokando ya barabara kuu ya Iringa Mbeya kuwa eneo la Malisho ya Mifugo jambo ambalo ni hatari kwa usalama wa abiria wanaotumia barabara hiyo.
Mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com mchana huu umeshuhudia kundi kubwa la ng'ombe wakiwa katika malisho eneo la Bhesania Ipogolo wakiwa katika malisho huku wananchi wakihoji uvunjaji wa sheria ya Manispaa ya Iringa .
Baadhi ya wananchi wameitaka manispaa ya Iringa kusimamia sheria hiyo ya mifugo kwa kuanzisha msako wa kukamata mifugo inayozagaa mjini ili kuepusha ajali .
Na Francis Godwin
0 comments:
Post a Comment