Msanii wa Kundi la Vichekesho, Mkwere kutoka kundi la Mizengwe akiigiza kama Askari wa Usalama wa Barabarani akisimamisha magari wakati wakitoa burudani katika Uzinduzi wa Wiki ya Nenda kwa Usalama iliyozinduliwa leo mjini Iringa katika Uwanja wa Samora. Maadhimisho hayo yameanza leo Septemba 17-22, 2012. Kaulimbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ni “PAMBANA NA AJALI ZA BARABARANI KWA VITENDO, ZINGATIA SHERIA”
Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Ndani. Dk. Emmanuel Nchimbi akisalimiana na Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama Barabarani Mkoa wa Iringa, Salim Ahmed Jabri Sasi, baada ya Waziri kuwsili uwanja wa Samora Iringa.
Waziri Nchimbi akisalaimMbunge wa Viti Maalum, Rita Moto Kabati na viongozi wengine wa Mkoa wa Iringa
Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mbando (kushoto) akimkabidhi Moderm ya Airtel 3.75G Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi wakati alipotembelea banda la kampuni hiyo ya Simu ambao ni wadha,mini wa Wiki ya Nenda kwa Usalama Kitaifa inayofanyika mkoani Iringa. Wengine katika picha ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani na Mwenyekiti wa Baraza la Usalama Barabarani. Pereira Silima (wapili kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dk. Christine Ishengoma. Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama yameanza leo kitaifa Mkoani Iringa.

Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi, akimkabidhi cheti cha heshima kwa kuwa wachangiaji katika kampeni ya kupambana na kupunguza ajali barabarani pamoja na Wiki ya Nenda kwa Usalama kitaifa, Meneja wa Airtel Kanda za Nyanda za Juu Kusini, Beda Kinunda.Makabidhiano hayo yalifanyika jana katika ufunguzi wa Wiki ya Nenda kwa Usalama Kitaifa mkoani Iringa.
Mkurugenzi Mkuu wa Makampuni ya ASAS, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Mkoa wa Iringa, Salim Ahmed, akipokea cheti cha heshima kwa kuwa wachangiaji katika kampeni ya kupambana na kupunguza ajali barabarani pamoja na Wiki ya Nenda kwa Usalama kitaifa, kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi. Makabidhiano hayo yalifanyika jana katika ufunguzi wa Wiki ya Nenda kwa Usalama Kitaifa mkoani Iringa.
0 comments:
Post a Comment