Mwandishi wetu, Iringa Yetu
SERIKALI mkoani Iringa imewapeleka waganga watano wa tiba za jadi nchini Burundi kupata utaalamu zaidi wa matumizi ya dawa za jadi, kwa lengo la kuwaongezea ujuzi wa matumizi ya miti shamba.
Akizungumzia hatua hiyo mwenyekiti wa Chama cha Waganga wa Jadi mkoani Iringa Dk, Galusi Msekwa, amesema serikali imewapeleka waganga hao pamoja na wale wanaotibu kwa kutumia mitishamba ili kuwawezesha kuendeleza taaluma yao ya kuwahudumia wananchi kikamilifu ili kuendana na wakati uliopo.
Dk, Msekwa amesema hatua ya kuwapeleka waganga hao wa jadi imekuja baada ya chama chao cha waganga wa jadi kusajiliwa na kutambuliwa rasmi na serikali hali ambayo imepelekea kuwepo kwa ushirikiano mkubwa wa kuyaboresha dawa za mitishamba ili itumike kisasa zaidi.
Watganga hao watasoma kwa muda wa wiki moja na watapatiwa ujuzi wa utayarishaji wa dawa za magonjwa mbalimbali ili kwenda kushirikiana na madaktari bingwa ambao wamebobea katika tasnia hiyo ya mitishamba.
Amesema waganga waliokwenda nchini Burundi wameteuliwa na Chama cha Waganga wa Jadi baada ya serikali kutoa nafasi hizo za kwenda kupatiwa mafunzo ya hatua za utambuzi wa madawa, utayarishaji, usindikaji, uhifadhi pamoja na matumizi ya dawa ambazo wagonjwa wao watakuwa wanahitaji.

Blogzamikoa
0 comments:
Post a Comment