Home » » WAZIRI LUKUVI AKABIDHI MSADA WA VITABU

WAZIRI LUKUVI AKABIDHI MSADA WA VITABU


NA OLIVER MOTTO- IRINGA

WAZIRI wa katiba, sera na uratibu wa bunge Mh. WilliumLukuvi amekabidhi vitabu kwa wanafunzi wa shule ya Wilium Lukuvi iliyopo
Magozi, Tarafa ya Pawaga katika Wilya ya Iringa, vitabu vyenye thamani
ya shilingi Milioni 6.8, kwa lengo la kuinua ufaulu wa wanafunzi
shuleni hapo.


Akikabidhi msaada huo uliotolewa na mfuko wa pensheni wa mashirika ya
Umma (PPF)  Mh. Lukuvi amesema msada huo umetokana na ombi la mkuu wa
shule hiyo, kutokana na tatizo hilo kuwaathiri wanafunzi.


Naye meneja uhusiano wa PPF, Bi. Lulu Mengele amesema hatua hiyo ni
moja ya utekelezaji wa sera ya mfuko huo wa mashirika ya Umma, katika
kushirikiana na serikali kuinua hali y elimu nchini.

Mkuu wa shule hiyo Bw. Charles Mgimwa amesema uhaba wa vitabu
umeathiri ufaulu wa wanafunzi shuleni hapo, kutokan na walimu kutumia
njia ya kuandika ubaoni pekee, na hivyo wanafunzi kukosa vitabu vya
kujisomea, na tatizo hilo lilikuwa nikwa vitabu vya masomo ya
Kiswahili,  Kiingereza, Jografia, Historia  na Uraia.

Aidha Mh. Lukuvi amewataka wanafunzi kuvitunza vitabu hivyo, ili
viwasaidie kwa muda mrefu huku akiwahimiza kujisomea na kuongeza
kiwango cha ufaulu.


Blogzamikoa

0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Iringa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa