Home » » TAHADHARI NOTI BANDIA ZAKAMATWA IRINGA

TAHADHARI NOTI BANDIA ZAKAMATWA IRINGA


Noti bandia zatua Iringa

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa Michael Kamuhanda akionyesha mfano wa noti za shilingi 10000 ambazo ni feki zilizokamatwa na jeshi la polisi zikiwa na thamani inayofanana na Tsh. zaidi ya 700,000

Jeshi la polisi mkoa wa Iringa limetoa tahadhari kwa wananchi kuwa makani na fedha wanazolipwa ili kuepuka kubambikizwa noti bandia ambazo tayari jeshi hilo limekamata zaidi ya bandia zenye thamani ya zaidi ya shilingi 700,000.


Kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa Michael Kamuhanda amesema leo kuwa noti hizo zimekamatwa na askari polisi baada ya kupata taarifa kutoka kwa wananchi wasamaria wema.


Kamuhanda alisema kuwa hadi sasa jeshi hilo la polisi linawasaka wahusika wa mtandao huo wa kusambaza noti bandia katika mkoa wa Iringa ili kuchukuliwa hatua za kisheria.


Alisema kuwa fedha hizo ambazo zimekamatwa katika maeneo tofauti tofauti zina namba ambazo zinafanana na hivyo kuwataka wafanyabiashara na wakulima kuwa makini na watu wanaofika kununua mazao yao .

Chanzo: Francins Godwin Blog

0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Iringa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa