na Gustav Chahe, Iringa
WATANZANIA wameshauriwa kuwa tayari kupokea mabadiliko ya kiteknolojia ifikapo mwishoni mwa mwaka, kwa kuwa huenda yakaathiri baadhi ya mawasiliano.
Mkurugenzi wa Tume ya Mawasiliano nchini, Addy Mkunze, alisema hayo katika warsha ya wadau wa habari, mkoani Iringa.
Alisema, tokea Julai mosi, 1951 Tanzania ilikuwa ikirusha matangazo yake kwa njia ya analojia ambayo imeonekana hayana ubora wa matangazo, wakati mwingine kuingiliana mara kwa mara.
Alisema katika mabadiliko hayo redio zitaendelea na matangazo yake kwa kuwa ni chombo muhimu kinachowagusa watu wa hali ya chini, lakini pamoja na hayo utafiti unaendelea kwa ajili ya mabadiliko.
Kwa mujibu wa mkurugenzi huyo, utangazaji wa kidijitali unakusudia kupunguza matumizi ya nishati kwani mitambo yake hutumia nishati ya umeme ndogo, kutumia muda mchache kutayarisha kipindi, kuwa na ubora wa sauti na picha, kuwa na vifaa vichache vya kuhifadhia habari nyingi na vipindi ikiwa ni pamoja na kuwa na maktaba ndogo ya kuhifadhi vipindi kulinganisha na vifaa vya analojia.
Alisema, Tanzania ni miongoni mwa nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki ambayo inatekeleza mpango wa kuboresha mawasiliano kutoka analojia kwenda dijitali ifikapo Desemba 31, 2012 mitambo ya analojia itazimwa.
Chanzo: Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment