Wanafunzi wa shule ya Msingi Mtwivila mjini Iringa wakifundishana wenyewe baada ya walimu wote kugoma
MGOMO wa walimu katika mkoa wa Iringa umeendelea kupoteza mwelekeo baada ya ya walimu kusalitiana na kupelekea walimu 765 pekee kati ya walimu 4,894 kugoma na idadi kubwa kuendelea na kazi.
Jumla ya walimu 989 wa shule za msingi na sekondari ndio waligoma na 6686 wagoma kuunga mkono mgomo huo.
Wakati shule kati ya shule za msingi na sekondari zilizogoma ni 95 kati ya shule 568 katika mkoa wa Iringa .
Uchunguzi uliofanywa na mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com katika shule mbali mbali mjini Iringa na nje ya Manispaa ya Iringa jana na leo umeshuhudia walimu hao wakiendelea na kazi kama kawaida huku wachache ndio ambao wameendelea na msimamo wao wa mgomo.
Hata hivyo idadi kubwa ya walimu wanadai wanasubiri maamuzi ya mahakama hapo kesho ndipo wataweza kutoa msimamo wao dhidi ya mgomo huo ila kwa leo wameona ni vema kuendelea na kazi kama kawaida.
katika shule ya Msingi Mlangali mjini Iringa walimu 16 kati ya 21 ndio ambao wamefika katika shule hiyo wakati shule ya Msingi Maendeleo walimu wamefika ila hawajaingia madarasani .
Afisa elimu mkoa wa Iringa Joseph Mnyikambi akizungumza na mwandishi wa habari hizi kuhusiana na hali ya mgomo huo alisema kuwa pamoja na baadhi ya mikoa hapa nchini idadi kubwa ya walimu kugoma na hata kufanya vurugu mbali mbali ila katika mkoa wa Iringa hali ni tofauti baada ya walimu kuonekana kuwa waelewa zaidi.
Mwinyikambi alisema kuwa kutokana na mgomo huo kuanza siku ya kwanza ambayo ni siku ya jumatatu uongozi wa mkoa wa Iringa ukiongozwa na mkuu wa mkoa wa Iringa Dkt Christine Ishengoma ulikutana na viongozi wa chama cha walimu Tanzania (CWT) mkoa wa Iringa na kufanya nao mazungumzo na viongozi hao kuonyesha uungwana na kukubali kusitisha mgomo huo.
Alisema kuwa katika mkoa wa Iringa kuna jumla ya walimu wa shule ya msingi 4,894 ila waliogoma ni walimu 765 idadi ambayo si mbaya sana .
Mwinyikambi alisema shule za msingi katika mkoa wa Iringa kwa maana ya wilaya ya Kilolo, Iringa vijijini ,Manispaa ya Iringa na Mufindi ni shule 465 na idadi ya walimu ni 4,894 na walimu 4,129 hawakugoma kabisa huku shule zilizo nyingi ziliendelea na masomo kama kawaida.
Katika Manispaa ya Iringa yenye shule za sekondari 26 ni shule 4 pekee ndizo ziligoma huku walimu wa sekondari waliogoma ni 224 kati ya walimu 393 na walimu wasiogoma ni 1568 .
Wakati katika wilaya ya Mufindi yenye shule za sekondari 41 shule zilizogoma ni 11 na walimu waliogoma ni 10 na wasiogoma ni 516 kati ya walimu wote 1,559 na wilaya ya Kilolo yenye shule za sekondari 22 shule zilizogoma ni 5 na walimu waliogoma ni 35 na wasiogoma ni 215 kati ya walimu wote 1,145.
Wilaya ya Iringa vijijini idadi ya shule za sekondari ni 27 walimu 1,407 shule zilizogoma ni 6 walimu waliogoma ni 34 na wasiogoma ni 489 .
Pia alisema kuwa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa ndio iliongoza kwa shule zake 30 kati ya 43 kugoma na walimu 360 kati ya 423 waligoma na kufuatiwa na wilaya ya Mufindi ambayo shule yenye shule 171 za msingi na shule 23 ziligoma na walimu 263 waligoma huku walimu 516 hawakugoma kati ya walimu 1,559 waliopo katika wilaya hiyo .
Wakati Halmashauri ya wilaya ya Iringa ilishika nafasi ya tatu kwa mgomo huo kwa kuwa na shule 9 zilizogoma kati ya shule 140 na walimu wake 74 waligoma na 489 hawakugoma kabisa .
Kilolo ilishika nafasi ya nne kwa shule kwa shule 7 kati ya 111 kugoma na walimu wake 68 kati ya 1,145 kugoma huku walimu 215,wakati Halmashauri ya Iringa vijijini ilishika nafasi ya mwisho katika mgomo huo kwa shule zake 7 kati ya 140 kugoma na walimu 74 kati ya walimu 1,407 huku walimu 489 hawakugoma .
Chanzo: Francis Godwin

0 comments:
Post a Comment