Home » » BAVICHA: SERIKALI IWEKEZE KATIKA KILIMO, VIWANDA

BAVICHA: SERIKALI IWEKEZE KATIKA KILIMO, VIWANDA


Mwandishi wetu, Iringa
Serikali imetakiwa kuwekeza katika kilimo na viwanda vya kusindika mazao lili kuweza kutengeneza ajira za uhakika badala ya jambo hilo kubaki kuwa ajenda ya wanasiasa wa chama tawala huku wakulima na sekta ya kilimo ikiendelea kuwa taabani.
Katibu wa Baraza la Vijana la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAVICHA), Deogratius Munishi amesema hayo wakati akihutubia wananchi wa Manispaa ya Iringa katika mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Mwembetogwa.
Munishi amesema mapinduzi ya uchumi kote duniani yameletwa na sekta ya kilimo kwa kusaidiwa na sekta ya viwanda ambapo sekta hizo huzalisha ajira kwa watu wa kada zote wasomi na wasio wasomi.

Naye Mwenyekiti wa baraza hilo, John Heche ametilia mashaka misaada ya wahisani mbalimbali inayotolewa kwa tanzania huku masharti yake yakiwa hayafahamiki kwa wananchi na kuongeza kuwa kutokana na mwenendo wa watendaji wengi serikalini kukosa uzalendo, taifa linaweza kujikuta mahali pabaya huku akitolea mfano ukuaji wa deni la taifa kutoka tirioni 7 mwaka 2005 hadi kufikia tirioni 24 mwaka huu
Viongozi hao wa bavicha wanaendelea na mikutano ya hadhara maeneo mbalimbali nchini kwa lengo la kueneza vuguvugu la mabadiliko au movement for change iliyozinduliwa na viongozi wao wa kitaifa mwaka huu huko arusha.
Blogzamikoa

0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Iringa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa